fbpx

Ulinzi imara kwenye kivinjari cha Chrome

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Unapozungumzia suala zima la usalama wa vifaa vya kidijiti katika dunia ya leo ni wazi kwamba kampuni mbalimbali zinafanya juhudi sana kuhakikisha bidhaa zao zinakuwa salama. Sasa kivinjari cha Chrome kimeboreshwa zaidi kiusalama.

Kama ulikuwa hufahamu ni kwamba kinjari cha Chrome ambacho kinaweza kutumika kwenye rununu/kompyuta kimeazimisha miaka kumi (10) tangu kuanzishwa kwake na katika maadhimisho hayo wahusika wameamua kuongeza ulinzi wa kutumia alama ya kidole.

Uboreshwaji huo wa kivijari hicho umekwenda mbali zaidi na unaweza kutambua sura (bila kusahau pua, macho na mdomo), msimbomilia zote na sentensi iliyoandikwa kwa Kilatini katika mfumo wa picha kwenye mtandao.

“Msimbomilia” ni Kiswahili fasaha cha neno barcode kwa Kiingereza.

kivinjari cha Chrome

Njia mpya ya ulinzi wa kutumia alama ya kidole kwenye kivinjari cha Chrome.

Google wametoa maboresho hayo kwa Android na iOS kwahiyo iwapo bado hujapokea masasisho cha kufanya ni kuhakikisha unatumia Chrome toleo la mwezi huu tarehe za karibuni kabisa.

Vyanzo: Engadget, The Verge

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  WhatsApp Business kwenye simu za iPhone
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.