fbpx
Android, apps, Intaneti, iOS, Teknolojia

Ulazima wa ‘Redeem Code’ kwenye rununu

ulazima-wa-redeem-code-kwenye-rununu
Sambaza

Wakati Google Playstore/App Store inawekwa kwenye simu rununu ni tofauti sana na mambo yalivyo hivi sasa na kuna mengi yamebadilika au kuboreshwa na moja kati ya vitu hivyo ni umuhimu/ulazima wa ‘Redeem Code’.

Kama unatumia simu janja inayotumia mfumo endeshi wa Android au iOS kwa namna moja au nyingine utakuwa umeshakutana na kutakiwa kuweka mchanganyiko wa neno siri ili kuweza kutumia App Store/Playstore.

Redeem” maana yake ni kuwa na uwezo wa kutumia kitu kwa mara nyingine tena baada ya uwezo huo kukosekana kwa kipindi fulani.

Sasa kwenye simu zetu pale unapofuta kila kitu kewenye simu au kwa lugha tuliyozoea “Restore“, baada tu ya kurudisha akaunti yako ileile iliyokuwepo hapo awali ukienda kwenye Playstore/ App Store itakudai Redeem Code“.

Redeem Code
Mchanganyiko wa namba amabao utatakiwa kuweka pale unaporudisha barua pepe iliyokuwepo hapo awali.

Redeem Code inapatikanaje?

Mtindo wa kutumia “Redeem Code” ulianza kuonekana kwa wale ambao wanatumia bidhaa za Apple lakini Google nao wakaona ni kitu kizuri hiyo wakaweka kwenye Android.

INAYOHUSIANA  Hoteli ya kwanza ya juu ya Anga kufunguliwa mwaka 2022

Kupatikana kwa namba hizo ni rahisi na kwa kuwa kitambulisho chako kwenye App Store ama Playstore ni barua pepe basi ujue kuwa mkusanyiko huo wa tarakimu utakuwepo kwenye barua pepe kupitia ujumbe uliotumwa na App Store/Playstore, Twitter, Google+.

Redeem Code
Jinsi inavyokuwe pale unapofanikiwa kuingiza tarakimu sahihi za kupata uwezo wa kutumia programu husika (iTunes).

Sasa usipate tabu tena/kuhuzunika pale itakapokubidi kuweka namba hizo kwenye kifaa unachotumia iwe simu janja, kompyuta, n.k.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|