fbpx
AirPods, Apple, Teknolojia

Ujio wa AirPods Pro 2020 wasogezwa mbele

ujio-wa-airpods-pro-2020-wasogezwa-mbele
Sambaza

Moja ya bidhaa za Apple ambazo zinaiweka sehemu nzuri ya kibiashara kamuni husika ni spika zake za masikioni ambazo zimetenegenezwa kwa teknolojia ya bila waya. Hata hivyo, ujio wa toleo jipya la AirPods Pro umepigwa kalenda!.

Wengi wetu tunafahamu fika kuwa toleo la kwanza kwa spika hizi za masikioni tayari lipo sokoni tangu mwezi Oktoba 2019 na ilitegemewa Aprili 21 2020 basi Apple wangezindua AirPods Pro 2020 lakini sasa shughuli hiyo imesogezwa mbele kutokana na sababu zisizozuilika lakini pia huu ndio wakati wa kununua bidhaa za kidijiti kwani nyingi zimeshuka bei.

Imeelezwa kuwa kutokana na ugonjwa wa homa ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona AirPods Pro 2020 zitazinduliwa mwanzoni mwa nusu ya pili wa mwaka huu ama hali ikiwa mbaya basi tutegemee kuziona mwaka 2021.

AirPods Pro 2020
Kwenye uzinduzi huo inatazamiwa pia kuzinduliwa kwa AirPods Pro Lite, AirPods X na Beats toleo jipya.

Kuna uwezekano wa MacBook Pro nyingine kutoka mwezi Mei lakini kwa bidhaa nyinginezo vyanzo vingi vinaeleza tutegemee kuziona kati ya mwezi Septemba/Oktoba mwaka huu. Taarifa hii imekuhuzunisha kutokana na shughuli kusogezwa mbele? Tupe maoni yako tafadhali.

TeknoKona tupo kila siku hivyo basi wewe msomaji wetu usisite kutembelea tovuti yetu mara kwa mara ili kuweza kusoma habari mbalimbali zinahusu teknolojia.

Vyanzo: iMore, Apple Insider

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  'Share' Mafaili Ya DropBox Ukiwa Katika App Ya Facebook Messenger!
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|