Samsung Galaxy M32 ni moja ya simu janja ambayo kwa muda tuu imekuwa ikitolewa dondoo zisizo rasmi kuhusu sifa zake lakini muda wa kufahamu kila kitu kinagaubaga umefika kwani rununu hiyo imezinduliwa huko India.
Simu hii ambayo kimsingi imejaa sifa za kuvutia inatazamiwa kupata wateja wengi hasa kutokana na kile kilichowekwa kwenye rununu husika kuanzia ubora wa kioo, kamera, uwezo wa betri, n.k. Fuatana nami kuweza kufahamu sifa za Samsung Galaxy M32.
Ubora wa kioo|Kipuri mama
Kioo cha simu hii kina ukubwa wa inchi 6.4, kina ung’avu wa hali ya juu sana halikadhalika upande wa kipuri mama rununu husika imewekwa Helio G80 SoC ikielezwa kuwa ni kifaa chenye nguvu, kasi kufanya mambo yawe mazuri.
Uwezo wa betri|Kamera
Kwenye dunia ya leo simu janja ikiwa na uwezo mdogo wa betri hakika mauzo yako hayatakuwa mazuri hivyo makampuni mengi wanajitahidi kila inapotoka simu janja basi iwe yenye betri kubwa. Samsung Galaxy ina mAh 6000, uwezo wa kuchaji haraka kwa 25W. kwenye upande wa kamera ya mbele ina MP 20, upande wa nyuma kuna kamera 4-MP 64, MP 8 na mbili zina MP 2.

Diski uhifadhi|Mengineyo
Kipengele cha memori kwenye simu janja huwa kina mvuto wa kipekee hasa katika ulimwengu huu wa kisasa zaidi. Simu hii inapatikana katika toleo mbili tofauti kwa maana ya kwamba RAM ni GB 4 au 6, diski uhifadhi-GB 64/128 lakini inawezekana pia kuweka memori ya ziada.

Julai 28 ndio simu hii itaingia sokoni ambapo bei yake ni $200 (4/GB 64)|zaidi ya Tsh. 430,000 au $230 (6/128)|zaidi ya Tsh. 529,000 bei ya ughaibuni na mauzo kuanzia Amazon.
Vyanzo: GSMArena, mitandao mbalimbali
One Comment