fbpx

Udukuzi WhatsApp: Udukuzi mkubwa umefanyika kwa watumiaji wa WhatsApp

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Udukuzi WhatsApp. Jumanne hii WhatsApp ambayo ipo chini ya Facebook imeomba usaidizi rasmi wa wizara ya Sheria ya Marekani katika uchunguzi juu ya udukuzi uliofanywa na watu wanaonekana kuwezeshwa na serikali.

WhatsApp wamesema huduma yao imefanyiwa udukuzi wa kupata nafasi ya kufikia mtumiaji yeyote wa WhatsApp na kuchunguza simu ya mtu husika bila mtumiaji simu kuwa na taarifa yeyote kama udukuzi huo unafanyika.

INAYOHUSIANA  Facebook Yaanza Kusapoti Mifumo Ya GIF Katika Picha Sasa!

Uchunguzi wao wa sasa unaonesha kuna teknolojia ya hali ya juu umetumika na hivyo wanaamini imehusisha kampuni binafsi yenye kupata msaada kutoka vyombo vya serikali. Wengi hadi sasa wanahisi itakuwa imehusisha makampuni ya Israeli.

Walengwa: Kwa watumiaji wa kawaida wengi wasiwe na hofu sana ila kwa wale ambao wanajihusisha na masuala ya haki za binadamu au mlengo wa kisiasa ndio watumiaji wanaodhaniwa watakuwa wamefanyiwa udukuzi ikiwa ni njia ya wahusika na udukuzi huu kuwafuatilia mambo yao.

INAYOHUSIANA  Motorola wametoa nyingine inaitwa Moto Z3

Udukuzi WhatsApp. Jumanne hii WhatsApp ambayo ipo chini ya Facebook imeomba usaidizi rasmi wa wizara ya Sheria ya Marekani usaidizi katika utafiti juu ya udukuzi uliofanywa na watu wanaonekana kuwezeshwa na serikali.  WhatsApp wamesema huduma yao imefanyiwa udukuzi wa kupata nafasi ya kufikia mtumiaji yeyote wa WhatsApp na kuchunguza simu ya mtu husika bila mtumiaji simu kuwa na taarifa yeyote kama udukuzi huo unafanyika.  Uchunguzi wao wa sasa unaonesha kuna teknolojia ya udukuzi wa hali ya juu umetumika na hivyo wanaamini imehusisha kampuni binafsi yenye kupata msaada kutoka vyombo vya serikali. Wengi hadi sasa wanahisi itakuwa imehusisha makampuni ya Israeli.  Walengwa: Kwa watumiaji wa kawaida wengi wasiwe na hofu sana ila kwa wale ambao wanajihusisha na masuala ya haki za binadamu au mlengo wa kisiasa ndio watumiaji wanaodhaniwa watakuwa wamefanyiwa udukuzi ikiwa ni njia ya wahusika na udukuzi huu kuwafuatilia mambo yao.  WhatsApp inawastani wa watumiaji bilioni 1.5 kila mwezi na suala hili litakuwa limewachafulia sifa kwani ni kwa muda mrefu wamekuwa wakisifia teknolojia za kiusalama walizoziweka katika app hii kwa sasa.  Watumiaji wote, wa Android na iPhone wanatakiwa kuhakikisha wasasisha WhatsApp haraka iwezekanavyo kwenda kwenye toleo la kisasa zaidi - wamesharekebisha eneo ambalo lilitumiwa kama njia ya udukuzi. whatsapp mwisho kupatikana

WhatsApp inawastani wa watumiaji bilioni 1.5 kila mwezi na suala hili litakuwa limewachafulia sifa kwani ni kwa muda mrefu wamekuwa wakisifia teknolojia za kiusalama walizoziweka katika app hii kwa sasa.

Watumiaji wote, wa Android na iPhone wanatakiwa kuhakikisha wasasisha WhatsApp haraka iwezekanavyo kwenda kwenye toleo la kisasa zaidi – wamesharekebisha eneo ambalo lilitumiwa kama njia ya udukuzi.

Download WhatsApp – Android Google Play

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.