fbpx
Sayansi, Uchina

Uchina kutengeneza Mwezi bandia

uchina-kutengeneza-mwezi-bandia
Sambaza

Mambo ya sayansi na teknolojia yanaendelea kukua na katika dunia ya leo Uchina wanatengeneza Mwezi bandia ambao unalenga kusaidia  kutoa mwangaza Kusini Magharibi mwa Chengdu.

Mpango huo ambao mpaka hivi sasa unaendelea kwa lengo ambalo wahusika wanaamini utasaidia katika kufanya Chengdu iwe na uhakika wa kupata mwanga mara nane zaidi kuliko mwanga wa hivi sasa unaotokana na Mwezi ambao sote tunaufahamu.

Mbali na kutoa mwanga wa ziada mwezi huo wa bandia utazunguka kwenye njia yake (Orbit) juu ya Dunia maili 310 kulinganisha na 236000mi mbali na sayari Dunia.

Mwezi bandia ukikakamilika unategemewa kuokoa gharama za umeme zinazokaribia $173m, ukosefu wa mwanga wakati wa majanga yasiyozuilika au pindi umeme unapokatika.

Mwezi bandia
Mwezi huo utaweza kuwekwa sehemu husika kwa kutumia satelaiti Xichang.

Mwezi huo unatarajiwa kuzinduliwa mwaka 2020 na iwapo itaonekana kuwa na msaada basi miezi mingine bandia kuzinduliwa mwaka 2022.

Vyanzo: ABC15 Arizona, South China Morning Post

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Misheni ya Juno: Picha ya kwanza ya Jupiter yatolewa
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|