fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

simu Tecno Uchambuzi

Uchambuzi wa Simu ya Tecno Camon 15, uwezo na sifa

Uchambuzi wa Simu ya Tecno Camon 15, uwezo na sifa

Spread the love

Kampuni ya Tecno inasifika kwa kutoa simu zenye thamani nzuri kwa pesa ya mnunuaji, zikiwa na faida kubwa kama kukaa na chaji kwa muda mrefu wa matumizi na pia kamera zenye ubora mzuri kwa matumizi mbalimbali ya upigaji picha. Simu hii ya Tecno Camon 15 inaendelea kuwa katika sifa hiyo ya thamani nzuri.

Simu ya Tecno Camon 15

Simu hii ilianza kupatikana Februari 2020

 

SOMA PIA  Simu ya Oppo F11 Pro toleo la pili! #Uchambuzi

Simu hii hupatikana kwa takribani shilingi laki nne za kitanzania. Kiasi hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mahali pa ununuzi.

Sifa za Tecno Camon 15.

  • Kioo (Display) cha teknolojia ya LCD chenye ukubwa wa inch 6.6
  • Mfumo Endeshi wa Android 10.
  • Chipset ya Mediatek Helio P22
  • RAM ya GB 4 na diski uhifadhi yenye ukubwa wa GB 64
  • Mfumo wa kamera nne nyuma (MP 48, 2, 2 na QVGA) na kamera ya MP 16 mbele
  • Betri yenye uwezo wa 5000 mAh
SOMA PIA  Meizu Zero: Simu isiyokuwa na mengi tuliyoyazoea

Simu hii ina teknolojia ya utambuzi wa alama za vidole (Fingerprint). Pia, ina teknolojia ya mawasiliano ya 4G kwa ajili ya mtandao wenye kasi na pia ina teknolojia za WiFi na Bluetooth kwa ajili ya kuhirikisha data na taarifa nyingine. Pia, ina huduma ya FM Radio.

 

Simu hii ina sehemu ya kuchomeka waya wa chaji aina ya microUSB 2.0 na sehemu ya kuchomeka waya wa earphones. Ina matoleo matatu ya rangi, Dhahabu (Shoal Gold), Zambarau (Fascinating Purple) na Kijani (Jade).

camon 15 camera

Camon 15 ni moja ya simu yenye kamera nzuri katika familia za simu za Tecno zilizoingia sokoni mwaka 2020

Fahamu kwa undani uwezo wa kamera yake kwa kusoma makala yetu hapa – Ifahamu Kamera Ya TECNO Camon 15!

Joshua Maige

Mkazi wa Dar es Salaam, Tanzania.
Kwa sasa, ni mwanafunzi katika Taasisi ya Teknolojia ya Dar es Salaam(DIT), pia ni mwandishi wa makala za kiteknolojia katika ukurasa wa Teknokona.

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania