fbpx

Ubora wa picha kwenye Nokia 9 PureView

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Kama umekuwa mfuatiliajo mzuri wa simu janja zinazobeba jina la Nokia utakubaliana nami kuwa wanaimarika kila mara wanapotoa bidhaa mpya sokoni; saa chache zijazo wanatazamiwa kuzindua Nokia 9.

Jumapili ya Februari 24 2019 kwenye onyesho la MWC19 litakalofanyika huka Barcelona-Uhispania. Simu hiyo inaelewzwa kuwa na mengi mazuri hasa ubora wa picha na ukizingatia kuwa na kamera 5 upande wa nyuma.

INAYOHUSIANA  Apps za wanyama zawekewa katazo kulinda usalama wa wnyama pori

 

Nokia 9 PureView

Muonekano wa mbele/nyuma pamoja na idadi ya kamera ambazo zipo kwenye Nokia 9.

Wakati watu wengi duniani kote wakisubiri kuweza kufahamu sifa inazobeba Nokia 9 PureView tayari vionjo ya uwezo wa kamera zake umeweza kubainika kulingana na picha ambacho imepigwa kwa kutumia simu husika kitu ambacho kimezua gumzo kuhusiana na ubora wa kamera zake zipatazo tano (5) kwa idadi.

Nokia 9 PureView

Picha+nakshi nakshi zote zimefanyika kwenye Nokia 9 PureView.

Sifa za Nokia 9 Pureview

  • RAM ya GB 6
  • Diski uhifadhi wa GB 128
  • Haipati shida ikilowa maji kidogo (waterproof – IP67)
  • Ukubwa wa inchi 5.99 (2K OLED)
  • Betri la mAh 3,320
INAYOHUSIANA  Nokia 3310 (2017) ina Tatizo litakaloifanya kutonunuliwa kwa baadhi ya Nchi #Uchambuzi

Bei ni za kimarekani dola 699 ambazo ni takribani Tsh Milioni 1.6 kwa bei ya kuagiza (ughaibuni) lakini pia imeelezwa kuwa rununu husika haitakuwa na mahali pa kuchomekea spika za masikioni kitu ambacho kimekuwa kikifanywa na makampuni mengi tuu.

Vyanzo: GSMArena, News 18, The Verge

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|