fbpx
Uber, Usafiri

Uber Kufungia Wateja/Wasafiri Wasumbufu!

uber-kufungia-wateja-wasafiri-wasumbufu
Sambaza

Kama kawaida lawama nyingi huwa zinawafikia maderva tuu ambao wanaendesha magari kwa kutumia Uber. Vipi kuhusu wateja wao sasa? ni mara chache sana utapata kusikia kuwa wateja hao wameshitakiwa.

Kazi kubwa inabakiaga tuu kwa madereva wa Uber ambapo huwa wanaadhibiwa na kampuni na hata wateja mufa mwingine katika sanduku la maoni huwa wanawatolea sifa mbaya (wanazostahili baada ya kukiuka makubalino/sheria) au hata kuto wapa nyota zao.

INAYOHUSIANA  Bombardier 'Kufyeka' maelfu ya wafanyakazi
App Ya Uber
Uber: App maarufu inayorahisisha huduma ya Taxi yenye kuzidi kuwa maarufu kila siku

Kwa madereva kupata maoni ya kusifiwa na kuwa na nyota za kutosha ni kitu cha msingi sana kwao kwani tangia mara ya kwanza wanavyojiunga na mtandao huo huwa wanaambiwaga.

Kwa mfano dereva ambae ana nyota chache sana na katika eneo lake la kuachia maoni lina malalamiko mengi kuhusu yeye basi Uber wenyewe wanaweza kuchukua jukumu la kumuondoa kabisa katika mtandao huo.

INAYOHUSIANA  Uber na Tigo zashirikiana kama njia ya kuwafikia wateja wao vizuri

Hii itakua ni hivyo hivyo hata kwa wasafiri ambao wanatumia Uber, ni wazi kabisa kuwa Uber wanaweza mfuta msafiri katika App yao baada ya yeye kwenda kinyume na taratibu pangwa.

App Ya Uber

Ukiachana na hayo pia Uber imweka wazi kuwa mabadiliko haya yataonekana kwa kiasi kidogo sana na hii ni kwamba watumiaji wengi wa Uber wana tabia ambazo zinafanana (wastarabu). Hii inamaanisha kuwa mabadiliko haya yatahusisha namba ndogo sana ya wasafiri.

Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment. Kama hiyo haitoshi usisite kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari kede kede za teknolojia na sayansi.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags:

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com