Ile kampuni maarufu kwa utoaji wa huduma wa taxi kwa njia ya kuita taxi kwa kutumia app (Uber app), sasa kufanyia majaribio gari zinazojendesha zenyewe zikiwa na abiria.
Kutokana na ukuaji wa soko la ushindani Uber wameamua kujaribu magari hayo ambayo yanaendeshwa bila ya uwepo wa devera. Hii itakuwa ni kwa mara ya kwanza tangu Uber ianze kutoa huduma ya taxi, mtumiaji atakuwa na uwezo wa kuchagua kama anataka huduma inayotolewa na Uber afuatwe na gari yenye dereva au la!
Magari hayo yatakuwa yakiamuriwa pakwenda pale mteja atakapobonyeza kwenye simu janja na kupelekwa mahali husika kulingana na ramani ya eneo analokwenda mteja. Hata hivyo gari hizo zitakuwa na dereva wa akiba kusaidia pale ambapo gari ya kujiendesha yenyewe haitaweza kujua la kufanya kukabiliana na jambo fulani.
Majaribio ya magari yanayojiendesha yenyewe hayataenda zaidi ya mji wa Pittsburgh na hakuna mpango wa karibuni kufanya majaribio kwenye miji mingine zaidi ya Pittsburgh.
Gharama za kutumia gari za Uber zinazojiendesha zenyewe zitakuwa ni rahisi zaidi ya mtu kumiliki gari yake na itakuwa ni bure kwa mteja yeyote atakayejitolea kutumia huduma taxi kwa gari linajiendesha lenyewe.
Pia Uber wametangaza tenda ya dola mil. 300 kwa Volvo kutengeneza magari yanayojiendesha yenyewe na kutoa ujuzi wa kilichonyuma ya pazia kwenye teknolojia ya magari yanayojiendesha yenyewe. Ielewe kuwa magari yanayojiendesha kutoka Uber yanatoka Ford. Uber wataanza kutumia magri hayo rasmi kwenye shughuli zake baadae mwezi huu.
Nini maoni yako kuhusu hatua ya majaribio ya magari yanayojiendesha kutoka Uber? Niambie katika sehemu ya comment. Hii ndio TeknoKona kwani daima tunakuhabarisha wewe msomaji wetu.
Vyanzo: Chicago Tribune, Vice news