fbpx

Twitter yapiga marufuku matangazo ya sarafu za kidigitali katika mtandao wake

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mtandao wa kijamii ya Twitter umetangaza kupiga marufuku matangazo ya sarafu za kidigitali (Cryptocurrency) na kuanzia jumanne hakutakuwa na matangazo ya sarafu hizo katika mtandao wake.

Twitter yapiga marufuku matangazo ya sarafu za kidigitali

Uamuzi kama huu tayari umeshachukuliwa na makampuni mengine kadhaa ya huduma za matangazo ya mtandaoni kama vile Google, na Facebook. Sababu kuu ambayo imetolewa na mitandao hiyo ni kwamba hatua hii inawasaidia kuwalinda watumiaji wa huduma zao dhidi ya udanganyifu au hasara inayoweza kutokea kwa kujihusisha na biashara hii.

INAYOHUSIANA  Kuna uwezekano Google kutengeneza simu yake mwaka huu! #Ripoti

Katika soko la mtandaoni, kuna sarafu 1587 za kidigitali ambazo ‘huchimbwa’ na kugeuzwa pesa halisi. Mifano ni Bitcoin, Ethereum, Ripple, Bitcoin Cash, LITECOIN na Cardano.

Twitter yapiga marufuku matangazo ya sarafu za kidigitali

Twitter yapiga marufuku matangazo ya sarafu za kidigitali katika mtandao wake

Marufuku hiyo inahusu ofa ya kwanza ya sarafu (ICOs) na mauzo, ilisema kampuni hiyo wakati wa mahojiano na Reuters Jumatatu.

Kampuni hiyo imepiga marufuku pia biashara za kampuni za sarafu hizo kutangaza biashara zao ikiwa hazijaorodheshwa katika soko la hisa linalofahamika.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya ku-unlock modem na kuweza kutumia sim card yoyote

Mpango huo utatekelezwa katika muda wa siku 30 zijazo. Kuanzia Juni, hakutakuwa na matangazo hayo kwa Google baada ya kampuni hiyo pia kupiga marufuku. Facebook kwa upande wake imedhibiti matangazo hayo katika mtandao wake.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.