fbpx
apps, Intaneti, Mtandao wa Kijamii

Twitter sasa kuhakikisha usalama kwenye mazungumzo

twitter-kuhakikisha-usalama-kwenye-mazungumzo
Sambaza

Kwa taarifa zilizotoka hivi karibuni zinasema kuwa Twitter wapo mbioni kutumia mtindo wa kulinda ujumbe wa watumiaji wake wa mazungumzo yao yanakuwa yanaweza kusomwa kati ya watu wawili tu.

Utaratibu huo (end-to-end) hufanya mazungumzo yote yanayofanywa na watu wawili kubaki kuwa siri bila ya kuweza kuingiliwa na mtu wa tatu.

Mjuzi wa kuandika programu mwenye jicho la Tai, Bi. Jane Manchun Wong pamoja na mitandao mbalimbali  amegundua hilo kupitia majaribio na uchunguzi alioufanya kwenye programu ya Twitter kwenye simu za Android.

usalama kwenye mazungumzo
Moja wa watu waliobaini kuwa Twitter ipo mbioni kuhakikisha jumbe za watu zinakuwa salama.

Mwaka 2016, Edward Snowden alimwomba Mkurugenzi Mtendaji wa Twitter, Bw. Jack Dorsey kuwa na uwezekano wa kulinda mawasiliano kati ya wale wanaowaliana (end-to-end encryption) kwenye Twitter au uwepo na utaratibu wa ujumbe kufutika pale tu muhusika aliyetumiwa atakapousoma.

usalama kwenye mazungumzo
Maana ya ujumbe kuweza kusomwa na wale ambao wanawasiliana tu.

Ombi la Snowden lilijibiwa na Mkurugenzi huyo kwamba inawezekana na watafikiria ushauri wake. Twitter inayojulikana sana kwa alama yake ya reli (hashtag) inaonekana kutekeleza ombi la Bw. Snowden kimya kimya.

INAYOHUSIANA  Maelfu ya watumiaji wa app ya SnapChat hawajapendezwa na sasisho jipya

Kuongezeka kwa kipengele hicho kutaizidishia Twitter kuwa jukwaa lililo salama zaidi kwa mawasiliano na ufikishaji ujumbe kwa jamii. Mpaka sasa Twitter haijatoa tamko lake kuhusiana na taarifa hiyo kama ina ukweli wowote au la!

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.