Twitter ina mambo mapya ya kuvutia

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Sio jambo ambalo limejificha kuhusu idadi ya watu wanaotumia mtandao wa kijamii wa Twitter au hata wale ambao wanafikiria kufungua akaunti huko na kuitumia. Hali hiyo huenda ikabadilika kutokana na mambo mapya ya kuvutia.

Kama utakuwa umepita kwenye akaunti yako ya Twitter kuna mabadiliko utakuwa umeyaona na kwa idadi ni vitu viwili vimeongezwa; mosi kuweza kufuatilia maoni kwa ukaribu zaidi na pili kujua kama mtu yupo hewani au la!.

mambo mapya ya kuvutia

Muonekano uliobireshwa unamuwezesha mtumiaji wa Twitter kuweza kufuatilia/kujibu maoni kiurahisi.

Ukiangazia suala zima la kutaka kujua iwapo mtu yupo hewani kwa muda huo inaweza ikawa ni hatua nzuri ya kuweza kujua yule unayemfuatilia yupo kwa muda huo au hayupo.

Suala la kuonyesha kuwa mtu yupo hewani linaweza lisiwavutie watu kwa wingi hasa pale ambapo Twitter itaamua kupa uhuru mwenye akaunti kuweza kuonyesha yupo hewani au vingineyo.

Vipengele hivyo sio vitu vipya lakini kimsingi ni kujaribu kuwasogeza watu karibu na mtandao huo wa kijamii kama ilivyo kwenye Facebook, Messenger, Instagram ambazo zinazidi kuwavutia watu kila leo.

Vyanzo: Wersm, SEJ

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Microsoft na Facebook kujenga mkongo wa Intaneti ktk Bahari ya Atlantic
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|