fbpx
Teknolojia, TV

TV kwenye chumba cha mtoto/watoto wako humsababishia kuongezeka uzito #Utafiti

tv-kwenye-chumba-cha-mtoto-athari

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163
Sambaza

Teknolojia inayokuwa kila leo pamoja na mapenzi kwa watoto vinaweza kuwa msukumo wa dhati na kukufanya ukamwekea mwao TV kwenye chumba anacholala, basi tambua kuwa jambo hilo si vyema kwa afya yake.

Katika miaka ya hivi karibuni na miaka mingi kwa wenzetu walipo kwenye dunia ya kwanza jambo la kuwepo TV katika chumba cha mtoto limekuwa si jambo la kustaajabisha. Katika utafiti uliofanywa na wanasayansi umebaini kuwa watoto wenye TV katika vyumba vyao vya kulala wana uwezekano mkubwa wa kuwa na uzito wa kupindukia kuliko wale ambao hawana.

INAYOHUSIANA  Vifaa Vya Muhimu Vya Kuwa Navyo Kwa Ajili Ya Simu Janja Yako!

Watafiti walibaini kuwa watoto wasichana kadri wanavyokaa muda mrefu wakitazama TV, ndivyo wanavyokuwa na uwezekano mkubwa wa uzito wao wa mwili kuongezeka.

Undani wa utafiti huo japo kwa uchache

Kwa muujibu wa jarida la International Journal of Obesity kuhusu unene wa kupindukia ulitathimini takwimu kutoka kwa watoto wadogo zaidi ya 12,000 nchini Uingereza. Wanasayansi hao walibaini kuwa zaidi ya nusu ya watoto waliokuwa na TV katika vyumba vyao vya kulala wakiwa na umri wa miaka saba.

Wasichana waliokuwa na TV ndani ya vyumba vyao vya kulalawakiwa na umri wa miaka saba walipatikana na 30% ya uwezekano wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia wanapofika umri wa miaka 11, wakilinganishwa na watoto wenzao ambao hawakuwa na TV vyumbani mwao. Kwa wavulana, hatari hiyo iliongezeka kwa 20%.

Soma pia: Matumizi ya simu gizani yanaweza kukusababishia kupoteza uwezo wa kuona

TV kwenye chumba cha mtoto
Tunawapenda watoto wetu ila si vyema wakija kuwa na uzito wa kupindukia.

Hatahivyo, watafiti wanasema hawawezi kuwa na uhakika kuhusu nini kinachosababisha uhusiano baina ya kutazama TV na kuongezeka kwa mwili, lakini wanasema huenda sababu ikawa ni watoto wenye TV vyumbani kusinzia kwa muda mfupi wakitumia muda mrefu kuitazama katika vyumba vyao vya kulala ama ulaji wa kiholela wanapotazama TV.

INAYOHUSIANA  Milango ya M-Pesa Yafunguliwa Kuruhusu Ubunifu

Wanasayansi pia hawakuacha kuwaangazia kundi jingine na kusema  kuna haja ya haraka sasa ya kuchunguza uwezekano huo (kuongezeka uzito) kwa watumiaji wa vipakatanishi (laptops) na simu za mkononi.

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|