fbpx

Trilioni 6 imetumika kununua maongezi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Watanzania milioni 41 wanaomiliki simu za mezani na mkononi wametumia zaidi ya shilingi trilioni 6 kwa ajili ya kulipia muda wa maongezi ndani na nje ya nchi pamoja na kutuma ujumbe mfupi wa maneno (sms).

Kiasi hicho cha matumizi kilirekodiwa kwenye robo ya pili ya mwaka iliyoishia Juni ni kikubwa ikilinganishwa na shilingi 4.8 trilioni zilizotumika katika kipindi kama hicho mwaka jana.

Hata hivyo, kiwango hicho kinaweza kupungua kutokana na baadhi ya mitandao ya simu kuwa na vifurushi vya maongezi na sms ambavyo ni kwa ajili ya promosheni ya kuvutia wateja zaidi.

trilioni 6

WAtanzania tunavyoneemesha mitandao ya simu za mkononi.

Kuongezeka kwa kiasi hicho ni kutokana na ongezeko la muda wa kupiga simu (dakika) na idadi ya ujumbe mfupi. Gharama nyingi isipokuwa kupiga simu nje ya nchi zilipungua katika vipindi hivyo vilivyofanyiwa uchambuzi.

INAYOHUSIANA  Nubia Alpha: Simu janja inayovaliwa mkononi

Ripoti ya mawasiliano kwa robo ya pili ya mwaka iliyotolewa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), inaonyesha mpaka sasa jumla ya watu milioni 41.8 wanatumia simu tofauti na kipindi kama hiki mwaka uliopita ambapo watumiaji walikuwa milioni 40.3.

Katika kipindi kilichoishia Juni 30, shilingi 4.4 trilioni zilitumika kama gharama ya muda wa maongezi, huku Tsh. 1.7 zikiwa ni gharama ya kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.