Je unafahamu ya kwamba simu yako inavijidudu vingi zaidi kuliko vilivyo kwenye kiti cha choo? ???????? Kama hufahamu basi fahamu sasa.
Suala hili ndilo limetumiwa na mtandao mkubwa wa huduma za intaneti nchini Japan ambao wameamua kuweka toilet paper kwa ajili ya simu janja kwenye vyoo mbalimbali katika moja ya kiwanja cha ndege maarufu huko nchini Japan.
Kampuni hiyo ya simu, Docomo, imeweka vidubwasha 86 vya kutolea toilet paper hizo katika vyoo mbalimbali katika kiwanja cha ndege cha Narita.
Wazo kuu la kuja na toilet paper hizo ni data tuliyoitaja juu inayoonesha ya kwamba simu za mkononi zinavijidudu (germs) mara tano zaidi ukilinganisha na idadi ya vijidudu kama hivyo vinavyopatikana katika eneo la kukalia katika vyoo vya kukalia.
Pia katika vikaratasi hivyo kuna ujumbe wa kibiashara ambapo wanatangaza ofa mbalimbali za intaneti wanazozitoa katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kwenye viwanja vya ndege.

Chooni ni moja ya sehemu ambazo Japan inasifika sana kwa kupafanya kuwa sehemu spesheli sana. Je ushasikia kuhusu vyoo vyao vyenye teknolojia ya kukusafisha vyenyewe? Soma hapa – Fahamu Vyoo Janja vya Nchini Japani
Vipi wewe unaonaje hili wazo lao hili ambalo kwa kiasi kikubwa linaonekana linafaida kubwa kimatangazo pia?
One Comment
Comments are closed.