Kama umezunguka zunguka mtandoani au hata katika simu janja yako ya Android ni lazima tuu neno APK uwe umepishana nalo, sina uhakika sana na Android App Bundle (AAB) maana hili limeanza kuonekana hivi karibuni
Kumbuka kwa kawaida tulikua tunashusha APK katika simu zetu kisha tunaziingiza katika simu zetu (Android) kwa ku’install ndio APK inabadilika inakua App kamili
Kwa kifupi baada ya kufanya hivyo ndio hapo unaweza kutumia App hiyo. Lakini kuna tofauti kubwa kati ya APK na AAB.
Google katika soko lao la Play Store kwa sasa wanahamasisha matumizi ya Android App Bundle (AAB) kuliko Android App Package (APK) huku sababu kamili ikiwa ni jinsi mifumo ya APK na AAB ilivyo
Ni wazi kuwa AAB ina mfumo mzuri na salama zaidi ukilinganisha na APK. unaweza ukajiuliza kwa namna gani sasa? ngoja nikuchambulie moja moja…..hahahaahaha
APK inafanya kazi hivi: inaunganisha kodi (code), mafaili mengimengi ambayo yanatosha kutengeneza App na kuyafanya kuwa kama katika file moja la ZIP.
Kumbuka file hili likiwa katika Playstore au mtandaoni pindi utakapolishusha na kuingiza katika simu yako halitachagua kwamba simu yako katika hayo mafaili (ulioshusha) kuna baadhi hayana maana kuingia au laa ……yote yataingia.
AAB inafanya kazi hivi: yenyewe hapa inakua imejitofautisha maana huwa kwa kawaida inakua na vipengele ambavyo ni lazima na vipengele ambavyo sio lazima katika mafaili yake. Vipengele hivyo vinaitwa “Dynamic Features” na “Asset Packs.”
Kwa kifupi ni kwamba hii ina kila kitu ambacho kinaweza tengeneza APK, Kwa maana kwamba ukishusha AAB kutoka playstore basi itaweza kujitengeneza APK ambayo mahususi na inaendana kabisa na kifaa chako Android.
Kwa maana nyingine ni kwamba unaweza kuwa na simu janja mbili za Android na ukawa na App moja kwa kila simu lakini bado App hizo zikawa zina utofauti wa kuandaliwa. Ni sawa na nyumba zinazofanana tuu.. lakini lazima ndani yake kuwe na utofauti tuu.
Naona Mpaka Hapo Somo Limefika!!!
Google kwa upande wao wanatoa kipaumbele sana kwa AAB kuliko APK, hili halimaanishi kwamba APK zitakuwa hazitumiki, ila kama AAB ikiwa inatumika sana basi tunaweza sahau kabisa.
Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini katika eneo la comment, niambie hii unaiona imekaaje?
Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.
No Comment! Be the first one.