fbpx

Thamani ya kampuni ya Apple imepanda

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Apple imekua kampuni ya kwanza kufikia thamani ya $1 trilioni ikiwapiku wapinzani wake kama Amazon ($877 bilioni), Alphabet ($858 bilioni), Microsoft ($817 bilioni) na nyinginezo.

Thamani ya soko la watengenezaji wa iPhone ilifikia kiwango ($1 trilioni) hicho mjini New York Agosti 2 2018 na hisa zake zilifikia rekodi mpya ya dola 207.39.

Hisa zake zimekuwa zikipanda tangu mwisho wa Julai 2018 wakati kampuni hiyo iliripotiwa kupata matokeo mazuri kuliko ilivyotarajiwa katika kipindi cha miezi mitatu kuelekea mwezi Juni.

Tangu iPhone ilipowekwa sokoni kwa mara ya kwanza mwaka 2007, hisa za Apple zimekuwa zikipanda kwa 1100% na kuongezeka takribani mara tatu katika kipindi cha mwaka uliopita.

Ongezeko hilo ni bora zaidi kwa kiwango cha 50,000% – tangu kampuni hiyo iliposajiliwa kwa mara ya kwanza mwaka 1980.

kampuni ya Apple

Hali kadhalika kuongezeka kwa hisa za Apple katika miezi ya hivi karibuni ulikuwa ni uamuzi wa kampuni hiyo wa kutenga $100bn za kununua hisa.

Chimbuko la Apple (kampuni).

INAYOHUSIANA  Tutegemee Earbuds zisizo na waya kutoka Beats mwezi Aprili

Apple ilianzishwa na muasisi mwenza wa kituo cha kutengeneza magari Steve Jobs mwaka 1976 na mwanzo ilifahamika zaidi kama kutengeneza kipakatalishi aina ya Mac kabla ya soko lake la simu janja kufungua njia ya uchumi wa programu tumishi.

Steve Jobs, ambae alifariki dunia mwaka 2011 na kurithiwa na Bw. Tim Cook (Mkurugenzi Mkuu wa sasa) amesimamia maendeleo ya iPhone, ambayo ilibadili kabisa kipato cha Apple.

Mapato yake yameongezeka.

Mwaka 2006, kampuni hiyo ilikuwa na mauzo ya chini ya dola 20 bilioni na kutangaza faida ya takribani dola 2 bilioni. Mwaka jana mauzo yake yalipanda hadi kufikia $229bn na faida ya $48.4bn, na kuifanya kuwa kampuni yenye faida kubwa zaidi miongoni mwa makampuni ya Marekani.

PetroChina iliwahi kuwa na thamani ya trilioni $1.1 kwa kipindi kifupi baada ya kuendesha shughuli zake mjini Shanghai in 2007, licha ya kwamba nyingi kati ya hisa zake zilishikiliwa na serikali ya Uchina; kwa sasa ina thamani ya takribani $220bn.

Uchambuzi.

INAYOHUSIANA  Visa kwenda Marekani hadi utoe taarifa zako za mitandao ya kijamii

Wakati masoko ya hisa ya makampuni mengine ya teknolojia yanahangaika, Apple iko mbele. Kupanda kwa hisa zake kumechochewa na mambo mawili muhimu:

Inauza simu chache za iPhone, lakini kwa kutengeneza simu zenye gharama kubwa mwaka jana, imeweza kutengeneza pesa zaidi kwa simu.

Apple pia ina vyanzo vingine vya mapato mathalani inatengeneza karibu $10bn kila baada ya miezi mitatu kutokana na mauzo ya programu tumishi, kuhifadhi data kwa njia ya kisasa zaidi pamoja na kusikiliza muziki bila kuupakua.

kampuni ya Apple

Programu tumishi mbalimbali zinazopatikana kwenye App Store.

Licha ya kupata thamani ya $1 trilioni wachanganuzi wa masuala ya kiuchumi bado hawaoni hisa za Apple kama ghali ikizingatiwa kwamba wanaendesha biashara ya takribani mara 15 ya faida iliyotarajiwa ikilinganishwa na ile ya Amazon ambayo ni mara 82 na mara 25 ya Microsoft.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.