fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Bitcoin Magari Sarafu za kidijitali Tesla

Tesla yakataa gari zake kununuliwa kwa kutumia Bitcoin

Tesla yakataa gari zake kununuliwa kwa kutumia Bitcoin

Spread the love

Moja ya makampuni makubwa yanayotengeneza magari yanayotumia nishati ya umeme TESLA ni mojawapo na mpaka hivi karibuni ilikuwa inakubali malipo kwa kutumia Bitcoin.

Bitcoin ndio sarafu ya kidjiti ambayo ni ghali kuliko zote hadi sasa lakini yenye inayokubalika kam njia mojawapo ya kufanya malipo sehemu nyingi duniani lakini hivi karibuni thamani yake imeshuka kiasi cha TESLA kupitia kwa Mkurugugenzi Mkuu Mtendaji, Bw. Elon Musk kusema kuwa kampuni hiyo haikubali tena watu kununua gari zao kwa kutumia Bitcoin.

SOMA PIA  Uganda: Mabasi ya umeme Jua kuanza kutengenzwa kwa wingi

Kupitia ukureasa wake wa Twitter, Bw. Elon Musk amesema kuwa wameangalia kwa karibu namna ambavyo Bitcoin ambavyo inavunwa kwa sasa na njia hizo zinaogopesha na mbaya sana kwa sasa.

kwa kutumia Bitcoin

Ujumbe wa Elon Musk kuhusiana na TESLA kuachana na mfumo wa malipo kwa kutumia Bitcoin.

Saa chache baada ya ujumbe huo wa Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TESLA hisa za kampuni hiyo zilishuka kwa 1.25% na mwezi Februari kampuni hiyo ilinunua Bitcoin zenye thamani ya $1.5 bilioni huku mwezi ulifuatia wakaanza kukubali malipo kwa kutumia sarafu hiyo ya kidjitali.

Takwimu zinaonyesha kuwa thamani ya Bitcoin hivi sasa imeshuka kwa karibu 12% jambo ambalo limesababisha Elon Musk kuweka wazi kusitisha kupokea malipo ya magari yao kwa Bitcoin.

kwa kutumia Bitcoin

TESLA yasitisha magari yao kununuliwa kwa kutumia sarafu ya kidjiti.

Je, TESLA watakubali tena njia hiyo ya malipo? Jibu ni ndio lakini itategemeana na uimara wa sarafu yenyewe sokoni lakini kwa sasa uamuzi ndio huo. Kumbuka kutufuatilia kila siku kwa habari mbalimbali za teknolojia kwa lugha adhimu ya Kiswahili.

Vyanzo: CNN, Gadgets 360

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.

Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania