fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

tecno

Gari Intaneti Teknolojia Tesla Usafiri

Tesla kupokea malipo kwa BitCoin, pia wawekeza zaidi ya $ Bilioni moja

Tesla kupokea malipo kwa BitCoin, pia wawekeza zaidi ya $ Bilioni moja

tecno

Kampuni ya magari ya Tesla kupokea malipo ya magari kwa sarafu ya Bitcoin. Hii itakuwa ni njia nyingine ya ziada nje ya malipo ya mfumo wa pesa uliozoeleka.

Katika taarifa iliyowekwa wazi kupitia taarifa yao ya wazi kwenda chombo cha kusimamia biashara za mfumo wa hisa nchini Marekani, SEC.

Tesla kupokea malipo kwa sarafu ya Bitcoin.

Kampuni ya magari ya Tesla kupokea malipo kwa sarafu ya Bitcoin.

 

Kampuni hiyo imesema imenunua bitcoin za thamani ya dola bilioni 1.5 za Kimarekani (Zaidi ya Tsh Trilioni 3.47). Kumbuka kampuni hiyo kufikia mwaka 2020 ilikuwa na kiasi cha pesa (cash) cha takribani dola bilioni 19 kwenye akaunti zake. Hivyo kuwekeza dola bilioni 1.5 ya pesa hizo kwenye bitcoin inaonesha ni kwa jinsi gani kampuni hiyo chini ya uongozi wa Elon Musk wanaamini sana mfumo wa pesa za kidigitali wa Bitcoin.

Bwana Elon Musk kwa muda sasa amekuwa akiwashauri watu wawekeze katika pesa za mifumo ya kidigitali kama vile Bitcoin. Ni siku chache tuu zilizopita aliongeza hashtag ya bitcoin kwenye akaunti yake ya Twitter, kujumlisha na jinsi anavyozungumzia masuala ya fedha hizi za kidigitali inasemakana katika kipindi cha hizi wiki mbili amechangia sana kukua kwa thamani ya pesa za kidigitali kama vile sarufu ya bitcoin na dogecoin.

SOMA PIA  Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu

Sarafu ya bitcoin imepanda thamani kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha wiki kadhaa sasa. Kufikia Jumatatu 8 Februari sarafu moja ya bitcoin ina thamani ya takribani dola 44,200 za Kimarekani – takribani Tsh Milioni 100, ukilinganisha na thamani ya dola 18,114.41 /Tsh Milioni 42 kufikia mwisho wa Novemba mwaka jana.

Soma zaidi kuhusu:

SOMA PIA  Acer waja na laptop 2 mpya: Nyembamba zaidi, na ya kwanza ya 'display' iliyopinda
Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania