fbpx
Android, apps, Usalama

Tenta Browser: Kivinjari salama kwa wasiotaka kufuatiliwa mtandaoni kwenye simu

tenta-browser-kivinjari-simu-android-vpn
Sambaza

Suala la usalama wa data za kimtandao limekuwa ni suala kubwa na nyeti sana kwa sasa. App ya Tenta Browser ni kivinjari cha Android kinachohakikisha usalama wa nyendo zako mtandao dhidi ya huduma za matangazo kama Google na huduma ya mtandao unayoitumia.

tenta browser

Kivinjari hichi kinafanya kazi kwa kutumia mfumo wa VPN – teknolojia ya VPN inahusisha kuficha taarifa tambulishi za watumiaji wa intaneti. Kwa kawaida unapotumia intaneti kuna kitambulishi cha kifaa unachotumia – kila kifaa kina namba tambulishi yake, pia kuna namba tambulishi ya mtoa huduma ya intaneti – mfano Tigo, Vodacom n.k.

INAYOHUSIANA  Backup and Sync: App/Programu Mpya ya Google Drive yaja

Kutokana na hili kumtambua mtumiaji anayetembelea tovuti flani kwa taarifa za anatokoa wapi n.k inakuwa rahisi. Kupitia VPN jambo hili linakuwa gumu. Fahamu zaidi kuhusu VPN hapa -> Teknokona/VPN

App ya Tenta Browser inakupa huduma hii kwa bure katika kivinjari chake. Ukihitaji huduma zingine za VPN kwa simu nzima ndio zinakuwa za kulipia.

App hii inaweza kukusaidia kufungua tovuti ambazo inawezekana ukifungua kwa kivinjari cha kawaida zinakuwa hazifunguki. Pia kivinjari kinakuja na uwezo wa kuzuia matangazo.

INAYOHUSIANA  Jinsi Ya Kuhamisha App Na Taarifa Zingine Kutoka Simu Moja Kwenda Nyingine!
tenta browser kivinjari vpn
Tenta Browser

Kivinjari hichi pia kinakuja na teknolojia za usalama kama vile ukekaji wa PIN (password) ila pia kama simu yako inateknolojia ya utambuzi wa alama za vidole basi unaweza kufungua app hii kwa mfumo huo pia.

Je unatumia kivinjari gani unapohitaji huduma ya VPN kwenye simu yako? Tuambie kwenye comment.

Download Tenta Browser -> Google Playstore

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |