fbpx

Browsing Category:Kompyuta

Wakati Microsoft Office 2010 tunaweza tukasema haijapata umaarufu kama ile ya 2007 kampuni ya Microsoft wapo njiani kuleta toleo jipya la programu hii.

Kitu kikubwa ni kuwa toleo hili litaweza kufanya kazi vizuri ata kwenye vifaa vya kugusa (touch screen), pia utaweza kusevu mafaili yako katika mfumo wa mawingu (kwa zaidi juu ya teknolojia hii unaweza soma makala kuhusu huduma ya Dropbox).
Microsoft Office hii itakuwa katika matoleo matatu, ambayo ni Office 365 Home Premium, Office 365 Small Business Premium, na Office 365 Pro plus.
Wakati Windows 8 inategemewa kuingia sokoni hapo Oktoba 26 kwa bei ya dola za kimarekani $ 40 (Takribani Tsh 63,000/=), hakuna tarehe au bei bado kwa ajili ya uzinduzi wa toleo jipya la Ofisi.
 
Ila toleo hili jipya ambalo hadi sasa wengi wanaliita Microsoft Word 2013 halitaweza kutumika kwenye kompyuta zinazotumia Windows XP na Windows Vista. Litaweza kutumika kwenye Windows 7 pamoja na toleo linalokuja la Windows 8.
 
Kwa habari zaidi;
 
0 Comments
Share
1212223