fbpx

Kuhusu:Kompyuta

Nilikuwa naichukulia kama moja ya gharama nafuu zaidi kwa watumiaji wakubwa wa kushusha(downloads) vitu toka mtandaoni. Kwa gharama ya Tsh 5,000/= kwa watumiaji wa modemu za 3G kupata huduma ya intaneti isiyo na kikomo kwa siku tatu na kwa ‘speed’ ya juu kabisa hata mimi nilijikuta nikitumia Zantel zaidi kwa mahitaji yangu yote ya ‘downloads’ kubwa.Ila siku chache zilizopita nilipotaka kujiunga tena nilikutana na kiwango kipya cha Tsh 10,000/= badala ya kile cha zamani cha Tsh 5,000/=, hii ikiwa ongezeko la asilimia mia.

Kwa kiasi flani naweza kuwaelewa lakini bado naamini  katika maamuzi ya kupandisha gharama za intaneti ya simu kufanya ambayo yameniumiza kwa kiasi flani hili ni moja wapo, likifuatiwa na la kampuni ya Airtel kuitoa ile bundle ya MB 400 kwa Tsh 2,500/=.

Kwa mtazamo mkubwa makampuni ya simu katika huduma za intaneti bado hayajafikia kiwango cha ‘fair price’/bei inayolingana na wanachotoa na tunacholipa, na kila inapokaribia hivyo kuna mtu mmoja anafanya maamuzi ambayo hayaathiri watumiaji tuu bali ata ‘customer loyality’.

Kwa malinganisho ya vifurushi vya intaneti kwa ajili ya wapenzi wa kushusha (download) vitu vikubwa kutoka intaneti kwa sasa nitashauri Zantel na Vodacom…


  • Vodacom ————>Kifurushi cha kutumia bila kikomo Siku 30——> Tsh 30,000/=

  • Zantel      ————>Kifurushi cha kutumia bila kikomo Siku 3  ——> Tsh 10,000/=

  • Vodacom ————>Kifurushi cha kutumia bila kikomo Siku7   ——> Tsh 10,000/=


Faida ya Zantel ukilanganisha na Vodacom ni kutokana na spidi ya juu isiyo na kikomo kwa Zantel wakati Vifurushi vya bila kikomo kutoka Vodacom vinashuka spidi hadi kati ya 25kb-35kb kwa sekunde hivi, kama kwako ni tofauti nitaarifu. Na je kuna Kifurushi gani kingine kutoka kampuni nyingine ya simu unadhani kipo bomba zaidi?

Kwa habari zaidi…Kwa Zantel www.zantel.co.tz  na kwa Vodacom
www.vodacom.co.tz
0 Comments
Sambaza
1181920