fbpx

Browsing Category:Intaneti

Bongoline, inapatikana kupitia anuani ya www.bongoline.com ni mtandao wa kijamii wa Tanzania. Upo hai kwa takribani mwaka mmoja na miezi mitatu~ (Proches Tairo ~Mwasisi wa Bongoline). Kuna mitandao mbalimbali ya kijamii yenye mizizi Tanzania, kama vile JamiiForums, ila nimevutiwa kuandika juu ya Bongoline. Naamini ni mtandao wenye uwezo wa kukua zaidi kwa kuwa una huduma nyingi na zenye kuvutia.
Kwa kuanzia mtandao huu unapatikana katika lugha mbili, unaweza kuchagua kuutumia katika lugha ya Kiswahili au Kiingereza kwa wale wapendao kimombo! Ukifungua www.bongoline.com utakutana na muonekano wa kwanza na wenye kuvutia.
BONGOLINE.COM
Nakumbuka miezi ya mwanzoni wakati nimejiunga na mtandao huu suala zima la muonekano (design) lilikuwa limefanana sana na Facebook, lakini wakafanya mabadiliko kadhaa makubwa yaliyoleta muonekano huu wa kipekee. Kwa kifupi ni kwamba Bongoline inahuduma nyingi sana zaidi hata ya Facebook na social site nyingine. Kuna Makundi (Groups), Blogu kwa ajili ya makala mbalimbali, huduma ya matangazo (hadi bure kwa siku saba), kushare ‘Documents’ na picha. Kitu kingine ni kwamba wamerahisisha kuunganisha huduma za Twitter na Facebook kwenye akaunti yako ya Bongoline. Kwa kuanzia unaweza ukajiandikisha moja kwa moja kupitia akaunti ya Facebook au Twitter.
TOLEO LA SIMU
Pia Bongoline ina toleo kwa ajili ya simu za mkononi, na kitu kizuri ni kwamba karibia simu za aina zote zenye huduma za mtandao zinafaa. Nimejaribu hata kwenye simu za kichina zenye huduma za mtandao na imekubali. Kitu pekee nilichoshidwa kuona ni sehemu ya ‘log out’ kwenye toleo la simu. Kama mtu yeyote akifanikiwa kupaona nijulishe.
Kulingana na Proches Tairo ni kwamba hadi sasa Bongoline ina takribani member 3,800. Je wangapi ni watumiaji wa mara kwa mara?
MAPENDEKEZO
-‘Log out’ kwenye toleo la simu iwekwe sehemu inayoonekana kirahisi
-Toleo la Kiswahili liboreshwe zaidi, sihamini kama vitu kama ‘Friend Request’, ‘Video Suggestions’ n.k vinashindikana.
-Kuwe na namna ya kutafuta marafiki ambao tayari ni ‘members’ kupitia vigezo vya miji, mapendeleo na n.k
TOLEO LA KISWAHILI
Naamini Bongoline ina uwezo wa kukua zaidi kupitia wingi wa huduma nzuri pamoja na mpangilio mzuri wa hudumu katika mtandao wao. Inabidi kuwekeza katika kujitangaza zaidi hasa kwa vijana na rika zingine.
Kuanzia masuala la siasa, michezo, burudani na biashara Bongoline ni mtandao wenye umuhimu kwa Watanzania kwa kuwa unavitu kwa ajili ya Watanzania, na hata kwa wale wasio Watanzania basi hapa ni sehemu ya kuwa karibu na Watanzania.
~Habari nilizopata toka kwa bwana Proches Tairo ni kwamba kutakuwa na mabadiliko ya muonekano (Design/Template) hivi karibuni, nategemea yatakuwa mazuri! #Pamoja Bongoline.~ www.bongoline.com
2 Comments
Share
1707172