fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti

IntanetisimuTanzaniaVodacom

Vodacom Waja na Ofa Kabambe!

Kampuni ya Vodacom masaa machache yaliyopita kupitia ukurasa wake wa Facebook wametangaza ofa kabambe kwa kipindi hichi cha mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Kuanzia saa tano usiku hadi saa moja wateja wa Vodacom wataweza kupiga simu bure(Vodacom kwenda Vodacom) na kutuma ujumbe mfupi wa maneno(sms) bila kikomo baada ya kujiunga kwa gharama ndogo ya Tsh 250/=…

Intaneti

Umoja wa Mataifa Watamka Intaneti ni Haki ya Binadamu

Hapo alhamisi, siku mbili zilizopita Baraza la Umoja wa Mataifa linalosimamia masuala ya Haki za Binadamu walipitisha azimio lililofanya kupata huduma za intaneti kama haki yako kama binadamu. Azimio hilo linasema watu wote wana haki ya kupata na kutumia huduma ya intaneti, pamoja na kujielezea kwa uhuru kupitia intaneti. Nchi 47 zote zinazotengeneza baraza hilo…

Barua pepeFacebookteknokona

Facebook Wazidi Kulaumiwa!

Tulishaandika kuhusu uamuzi wa ajabu uliochukuliwa na mtandao wa kijamii wa Facebook wa kubadilisha anuani za barua pepe katika profaili za watu wote. Hatua hii inafanya watu mbalimbali waliokuwa wanategemea kuunganisha program zao kama simu, laptop na huduma zingine katika kupata data muhimu kama barua pepe za watu wamekuta vitabu vya anuani (address book) zimebadilishwa….

FacebookMtandaoTanzania

Facebook Wabadilisha Anuani Ya Barua Pepe Yako Bila Taarifa!

Ndiyo, hicho ndicho kilichotokea. Miezi kadhaa iliyopita Facebook walizindua huduma ya barua pepe ambayo hakuna watu walioishabikia sana kwani wengine hata hawakutambua uwepo wake, kwa maana bado watumiaji wa Facebook hawakuhamisha matumizi yao ya barua pepe kutoka huduma makampuni kama Gmail au Yahoo.  Sasa Facebook wamebadilisha anuani za barua pepe kwenye ‘Profile’ za watumiaji wake…

JIEPUSHE Na Ku’click ‘Link’ Zisizo Na Maana Kwenye Mitandao Ya Kijamii!!
FacebookTanzaniaTeknolojia

JIEPUSHE Na Ku’click ‘Link’ Zisizo Na Maana Kwenye Mitandao Ya Kijamii!!

Siku chache zilizopita nilishangaa kupata mfululizo wa updates Facebook nikiambiwa rafiki yangu mmoja ameni’tag’ kwenye video flani. Kuja kuangalia ukurasa wangu wa Profile Facebook ilibidi nianze kazi ya ziada ya kuzifuta video hizo, kwani ilikuwa inaonesha picha ya ngono huku ikisema nitamchukia Rihanna kama niki’click link hiyo kwenda kuangalia hiyo video.

FacebookTanzaniaTeknolojia

Unaonaje Hii?

Nimeiopata hii toka gazeti la ‘online’ la Mashable [www.mashable.com]. Najua kwa Tanzania wengi wetu huwezi tuambia chochote kuhusu huduma nyingine za kijamii kama Google Plus na Twitter, wengi hatupo tayari kujaribu kitu kingine zaidi ya Facebook, na pale tunapojaribu tunakata tamaa mapema kwa sababu tunataka tukielewe na kuweza kutumia haraka zaidi. Lakini si kwa wenzetu…

TeknoKona Teknolojia Tanzania