fbpx

Teknolojia ya magari ya umeme yaingia Serengeti

0

Sambaza

Teknolojia ya magari ya umeme kwa ajili kutoa huduma za utalii imetambulishwa rasmi kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Teknolojia hiyo inatajwa kuwa rafiki wa mazingira na uhifadhi kwa kuwa magari hayo hayana kelele za ngurumo sanjari na ukweli kwamba hayatoi moshi kama ilivyozoeleka kwa magari mengine yanayotumia mafuta.

Hayo yamebainika baada ya Kampuni ya Mount Kilimanjaro Safari Club inayojishughulisha na utoaji wa huduma za utalii kutambulisha teknolojia hiyo kwa kuanza na magari mawili na imesema katika hatua za awali imeonyesha mafanikio makubwa.

Teknolojia ya magari ya umeme

Teknolojia hiyo ni nzuri kwani gari linakuwa jepesi na halitoi moshi jambo ambalo ni salama kwa hifadhi na lina uwezo wa kudumu kwa muda mrefu huku kinachohitajika ni wewe kuwa na uwezo wa kuchaji kila betri inapopungua.

Kwa Tanzania na imekuwa na ugumu kiasi lakini nchini Ujerumani ni teknolojia iliyozoeleka na yenye kutumiwa na watu wengi.

Iwapo mmiliki wa gari anahitaji kubadili kutoka kwenye kutumia nishati ya mfuta na kuweka teknolojia hiyo ya umeme ni lazima mfumo wote katika gari husika ubadilishwe na ni kwa gari lolote.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uwekezaji katika sarafu ya za kidijitali nchini Tanzania
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.