Mambo yanabadilika na vitu vipya vinatoka kila leo; sasa hata kama simu haipo katika kundi la kutambulika kama simu janja basi itakuwa na kamera kuifanya iweze kuvutia na kuuzika kwa watu/mataifa mbalimbali.
Mambo yalivyo hivi sasa simu janja ni lazima iwe na kamera angalau mbili ili kuweza kuwa katika nafasi nzuri ya kuwa katika usindani lakini bado ikaonekana hiyo haitoshi na siku hizi si kitu cha kushangaza kuona kamera 3-4 kwenye simu moja.
Mambo yapo mbioni kubadilika na kampuni, Light iliyojikita katika utengenezaji wa kamera ipo mbioni kuja na simu janja yake ambayo itakuwa na kamera 5-9 na kamera zote hizi zitakuwa kwenye simu moja.
Simu hii inaelezwa kuwa itakuwa na uwezo wa kupiga picha za ubora wa MP 64 bila kutumia kiasi kikubwa cha mwanga (flash).
Light wanafamika sana kwa bidhaa ya L16 (kamera 16 ndani ya kamera moja) ingawa kwa simu hii ambayo bado inatengenezwa inaonekana kuja kuifanya tena kampuni ikawa haabri ya muda mrefu vinywani mwa watu.
yazo: TechCrunch, The Verge, Hindustan Times
Timu ya uandishi wa Kona ya Teknolojia ingefurahi kupata sapoti yako ili iendelee kukuletea habari na maujanja mbalimbali.
Wezesha bando kwa kutuma kiasi chochote kupitia Selcom, kwenye simu yako bofya *150*50*1# kwenye namba ya malipo weka 60751369 jina litakuja TEKNOKONA.
Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia.
Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|