fbpx

CEO Wa OnePlus Asema Haya Tuyategemee Kutoka Kwao!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Inafahamika kuwa OnePlus ni kampuni kubwa ambayo inajulikana katika soko la simu janja. Kampuni imejibebea umaarufu mkubwa baada ya kutoa simu janja zake ambazo zina hadhi ya juu na pia zinaweza kushindanishwa na simu zingine.

Teknolojia ya simu inabadilika sana, kumbuka Samsung wanakuja na simu janja ambayo inakunjika (foldable). kwa upande wa OnePlus wao hawana papara kabisa  na jambo hili ….. ndio kwanza wanafikiria vitu vingine kabisa.

OnePlus 6 Ikiwa Inazinduliwa

Mkurugenzi mkuu wa OnePlus, Pete Lau amesema kwamba “Simu za kujikunja skrini sio sahihi sana kutoka kwa kipindi hichi kwani hakuna kitu ambacho ni kikubwa sana inachofanya ambacho ni tofauti na simu za kawaida…. ukiachilia mbali bei”

Hivyo basi kampuni inafikiria mambo mengine kede kede ambayo itawafanya kwa namna moja au nyingine kujitanua katika biashara. Hii inamaanisha ni pamoja na kuanzisha bidhaa zingine kama vile, Magari ya umeme, Tv janja na mengine mengi,

Maeneno hayo alisema wakati anahutubia katika chuo cha European Institute of Design, huko Italy. Hapa alijaribu kuelezea mambo ambayo wanayategemea mbeleni katika kampuni ya OnePlus.

Bado alisisitiza kuwa kuna uwezekano mkubwa kampuni ikaanza kutengenza vifaa vya kiletroniki kwa ajili ya ofisi ambavyo kwa ujumla vitakua na teknolojia ya 5G na AI.

Tv iko mbioni kutangazwa rasmi lakini biashara nyingine kama magari zitachukua muda kidogo, vile vile kutengeneza na kuuza simu kupo pale pale.

Ningepeda kusikia kutoka kwako. kampuni hili linapiga hatua nzuri, je unahisi litaweza kushindana na makampuni makubwa na kuchukua namba zao katika soko?

Tembelea TeknoKona Kila Siku Ili Uhabarike Na Habari Kibao Zinazohusu Teknolojia Kwa Ujumla, Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.