fbpx

TECNO Kwa Kushirikiana Na Klabu Ya Man City, Wanakuja Na Simu Janja!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kampuni ya simu maarufu ya Tecno iliingia ubia na Klabu kubwa duniani ya Manchester City mwaka 2016.  Katika ushirika huo inasemekana makampuni yote mawili yamekaa chini na kufikia muafaka wa kutoa simu janja ambayo itakua na chapa za makampuni yote mawili.

Ni jambo zuri sana kwani Tecno moja kwa moja wataweza kuwafikia mashabiki wa dhati wa Man City kwa kuwapa kile ambacho wamekitegemea kwa muda mrefu na pia hata wale wateja wao wa kila siku watapata kitu kipya.

Simu Ya Tecno Toleo La Man City

Inayosemekana Kuwa Ni Simu Ya Tecno Camon CX Toleo Maalamu La Man City

Kujua Ubia Huo Zaidi Ingia Hapa

INAYOHUSIANA  WhatsApp kupambana na taarifa za uongo

Lengo ni kuleta bidhaa ambazo zitakuwa na uhusiano wa moja kwa moja na klabu hiyo. Bidhaa ambayo itatumika si nyingine bali ni simu kutoka Tecno ya toleo la Camon CX.

Toleo la Camon CX  ni moja kati ya matoleo ya simu za Camon kutoka Tecno. Sifa kubwa katika simu janja hizi ni kwamba huwa zinakuja na kamera kali zaidi.

Simu Ya Tecno Toleo La Man City

Muonekano Wa Mbele Na Nyuma Wa Simu Hiyo

Kwa haraka haraka taarifa zilizopo ni kwamba simu itakuja na kamera yenye MP 16. Kamera ya mbele itakua na flashi mbili. Teknolojia ya alama za vidole itakuwepo ambayo itaweza kuhakikisha kuna usalama wa juu katika kifaa chako.

INAYOHUSIANA  TCRA wapunguza viwango vya gharama za kupiga simu 2018

Inasemekana mtu atakuwa na uwezo wa kupiga picha kwa haraka/kasi zaidi  yaani kwa kutumia sekunde 0.1 tuu

Muonekano wake utakuwa ni wa kijanja zaidi na ukiwa ndani  ya simu utaweza kutumia angalau App 50 bila ya simu kugandaganda (Stuck) kwani ina RAM ya GB 4.

Sifa zingine za undani tutakujuza kwa kina katika siku za usoni.

Simu Ya Tecno Toleo La Man City

Nembo Ya Man City Katika Simu Hiyo

Katika upande wa bei hatuna tatizo na Tecno, japokua hatujaijua lakini tunachojua ni kwamba simu za Tecno huwa zinakuja na hadhi kubwa na kuuzwa kwa bei ndogo

INAYOHUSIANA  BlackBerry yafikiria Kuachana na biashara ya Simu - bado hawatengenezi faida

Ningependa kusikia kutoka kwako, Una shauku ya kutaka kujuaa sifa za undani za simu hii?  Vile vile niandikie hapo chini sehemu ya comment, Niambie toleo gani la simu ya Tecno ambalo umeshawahi kutumia.

Kumbuka Kutembelea Mtandao Wako Pendwa Wa TeknoKona Kila Siku Kwani Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.