fbpx

simu, Tanzania, Teknolojia

Tecno kuzindua Spark 5 Pro yenye memori kubwa

tecno-kuzindua-spark-5-pro-yenye-memori-kubwa

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Soko la simu limekuwa limekuwa na ushindani mkubwa na kupelekea makampuni ya simu kuja na mbinu mpya za kujizolea wateja. Tukiongelea makampuni pendwa ya simu Afrika hatuezi kuacha kuipongeza kampuni ya simu ya TECNO.

Tunafahamu TECNO ina matoleo mbalimbali kama vile phantom, Camon, L series, Spark Series na mengineyo, na yote ni matoleo pendwa kutokana kuwa na sifa zenye kuvutia kama vile kamera nzuri, battery kubwa. lakini kati ya matoleo yote toleo la Spark limeonekana kupendwa sana labda hii ni kutokana muonekano mkubwa, utendaji maridhawa na bei isiyomuumiza mteja.

Pengine msomaji unaweza kujiuliza kwanini nmeamua kuizungumzia TECNO hususani TECNO Spark 5 pro ambayo ipo mbioni kuja na kwanini tutaepukana na ununuzi wa memori ya ziada ili kukidhi mahitaji yako.

Nikiwa kama mfuatiliaji wa masuala ya teknolojia na simu janja kwa ujumla nikapata wasaa wa kutembelea kwenye ukurasa wa Instagram- @tecnomobiletanzania na kukutana na picha ya Spark 5 pro yenye sifa zenye kuonekanika kama kioo aina ya Dot in Display cha takribani nchi 6 au 7 si chini ya hapo, nyuma ikiwa na kamera 4(16MP+2MP+2MP+AI Lens) na MP 8 za selfie. Kutokana na sifa hizo chache TECNO Spark 5pro ni mkali wa Spark zote za awali.Spark 5 Pro

INAYOHUSIANA  Angani kwa siku tano kwenye ndege ya abiria

Katika siku za usoni tutaleta uchambuzi kuhusu Tecno Spark 5 Pro na endelea kutufuatilia kila inapoitwa leo kwa habari mbalimbali zinazohusu masuala ya teknolojia.

Chanzo: Tecno

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Mato Eric

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Reply your comment

Your email address will not be published. Required fields are marked*