fbpx

TCRA kuzifutia leseni DSTV na ZUKU

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tangazo Agosti, 7 2018 la kusudio la kusimamisha leseni zilizotolewa kwa MULTICHOICE TANZANIA LIMITED (Dstv) na Simbanet Tanzania Ltd (ZUKU) kwa kushindwa kutekeleza amri halali za TCRA.

Aidha, kusudio la TCRA kwa kampuni hizo mbili ni kushindwa kutekeleza masharti ya leseni ikiwa ni pamoja na kjumuishwa kwa chaneli ambazo zinapaswa kuonyeshwa bure kwenye vifurushi vyao.

Simbanet Tanzania Limited, Multichoice Tanzania Limited, hairuhusiwi kuonyesha chaneli za televisheni zenye leseni za kutazamwa bila malipo kupitia ving’amuzi vyao isipokuwa TBC1 peke yake~TCRA.

DSTV na ZUKU

Tangazo la TCRA linalokusudia kuzifungia kampuni za Multichoice Tanzania LTD na Simbanet Tanzania LTD na kwa mujibu wa mamlaka husika walishawahi kuambiwa lakini wakakaidi agizo.

Tutegemee kuona mabadiliko kutoka kwa DSTV na ZUKU kwani sidhani kama watapenda wafutiwe leseni ya utoaji huduma.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Usajili wa kadi za simu kwa njia ya alama za vidole kuanza Mei Mosi 2019 #Tanzania
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.