fbpx

Tanzania, Teknolojia

TCRA kuinyang’anya leseni StarTimes

tcra-kuinyanganya-leseni-startimes

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Sambaza

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA imetoa tangazo la kuufahamisha umma wa watanzania kusudi la kuinyang’anya leseni kampuni ya Star Media Tanzania Limited (StarTimes) kwa kukiuka masharti ya leseni waliyopewa.

Tarehe 8 Juni 2010, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ilitoa leseni kwa kampuni ya STAR MEDIA TANZANIA LIMITED kwa ajili ya kurusha matangazo kidijitali.

Leseni waliyopewa StarTimes inahusisha kuonyesha chaneli za ndani kwenye ving’amuzi vyao na hazipaswi kulipiwa. Chaneli ambazo zinatakiwa kuangaliwa bure hata kama hujafanya malipo ya kifurushi chochote ni TBC1, ITV Channel 10, Clouds TV, Star TV na EA TV.

Hata hivyo, kwa muda mrefu imebainishwa na TCRA hasa baada ya malalamiko ya watazamaji wengi kutofurahishwa kwa chaneli hizo kutokuwa hewani pindi kifurushi kinapokwisha muda wake.

Utakumbuka siku chache zilizopita TCRA ilitoa taarifa kuhusu nia ya kufuta leseni za Simbanet Tanzania LTD (ZUKU) na Multichoice Tanzania LTD (DSTV) kujishwa kwa chaneli za bure kwenye malipo ya vifurushi mbalimbali huku Azam Media wakijihami kwa kuziondoa kwenye king’amuzi chao.

startimes
King’amuzi cha Starimes nacho imefikiwa na rungu la TCRA.

Suala la kutozwa pesa kwa chaneli za bure kwenye ving’amuzi vya StarTimes limekuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu na watumiaji wengi wa ving’amuzi vya kampuni hiyo, sasa TCRA wamejibu vilio vya wengi.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ifahamu Tecno Phantom Z Mini (V7), Uwezo wa Juu kwa Bei ya Kawaida
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.