fbpx

Intaneti, Mitandao ya Simu, TCRA

TCRA Yatakiwa Kumaliza Madai Juu Ya Ulanguzi Wa (Vifurushi) Bando Za Simu Na Internet! #Tanzania

tcra-kufuatilia-madai-ya-ulanguzi-wa-bando

Sambaza

Ni wazi kumekuwa na malalamiko mengi sana kuhusiana na bando za simu. Malalamiko mengi yamekuwa yakihusina na bando la internet.. kwamba wateja wanaweka bando hizo na zinawahi kuisha. TCRA na wizara husika zina tamko gani?

Malalamiko hayo hayo yamekuwa yakihusisha makampuni yanayotoa huduma hizo (mfano tigo, airtel, halotel n.k). Watumaiji wamekua wakilalamika kwamba wanaibiwa aidha ikiwa kwa njia ya vifurushi vyao kuisha katika hali ya sintofahamu

SOMA PIA  Piga simu kwa watu wengi kwa njia ya WhatsApp

Ukiachana na hayo kuna muda huduma inakua mbovu kiasi kwamba halii inapelekea bando kuisha muda wake wa kutumiwa bila hata ya mteja kutolitumia

Picha Na Daily News
Picha Na Daily News

Kingine ni kwamba bado kuna malalamiko kwamba makampuni hayo yanatoza gharama kubwa katika vifurushi vya intaneti na hata vile vya kupiga na kupokea simu (ongezeko hili hata mimi nimeliona ahahaha!)

Waziri wa  mawasiliano na teknolojia ya habari Dk. Faustine Ndugulile ametoa elekezo kwa mamlaka ya mawasiliano na habari TCRA kwamba jambo hili lipatiwe muarobaini mapema sana

Waziri pia amesema kuwa inabidi TRCA ianzishe mfumo wa uhakika na shutuma hizo kwa kufuatilia gharama wa kujua gharama halisi ya mawasiliano na kiasi ambacho wateja wanalipia.

Watanzania sio  wajinga, wanahitaji kujua thamani ya pesa zao katika bando hizo” —- aliendelea kusema waziri

Kingine cha kushangaza ni kuwa katika repoti iliyotolewa na ‘ICT Africa Internet’ inasema kuwa Tanzania ndio nchi ambayo ina gharama ndogo katika bando za intenet kwa africa mashariki.

SOMA PIA  Instagram yazindua IGTV. IGTV ni nini?

Somo Zaidi Habari Za TRCRA hapa!

Vyanzo ni DailyNews & Allafrica

Ningependa kusikia kutoka kwako, Hii unaionaje je ndio itakua suluhisho au wewe unahisi nini kifanyike? niandikie hapo chini kwenye sanduku la maoni.

Kumbuka Kutembelea mtandao wako pendwa wa teknokona kila siku kwani daima tupo na wewe katika teknolojia!

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Sambaza

Hashiman (@hashdough) Nuh

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

    Toa Maoni

    Your email address will not be published. Required fields are marked*