fbpx
Teknolojia

TCL na Android TV: TV za bei nafuu zinazotumia Android TV zaanza kupatikana

tcl-na-android-tv-tv-za-bei-nafuu-zinazotumia-android-tv-zaanza-kupatikana
Sambaza

TCL na Android TV za bei nafuu. Kampuni ya TCL ni moja ya makampuni makubwa duniani katika sekta ya utengenezaji na uuzaji TV.

TCL ni moja ya makampuni makubwa duniani katika utengenezaji wa TV za kisasa. Kwa mwaka 2019 ilikuwa ni kampuni namba mbili katika utengenezaji na usambazaji wa televisheni duniani. Kwa mwaka 2019 walikuwa na asilimia 13 ya soko la TV wakiwa nyuma ya Samsung mwenye asilimia 17.8.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kuzuia Mialiko ya Magemu kwenye Facebook

TCL hivi karibuni wametambulisha TV mpya janja za bei nafuu sana na zimeanza kupatikana nchini Marekani na huku ikitegemewa kuanza kupatikana pia katika mataifa mengine.

TV hizo zipoje?

Kuna ya ukubwa wa inchi 32 ikiwa inakuja na kiwango cha HD cha 720p, huku ya ukubwa wa inchi 40 ikija na ubora wa kiwango cha HD cha 1080p (Full HD).

Pia zinakuja na teknolojia zingine muhimu kama vile ubora wa sauti kwenye teknolojia ya Dolby Digital plus, WiFi na porti mbili za HDMI. TV zinapatikana kwa jina la familia ya ‘TCL 3-Series’.

INAYOHUSIANA  Makala na Habari za Wiki ya Novemba 10

Android TV

Kikubwa katika TV hizi ni uwepo wa toleo la programu endeshaji la Android TV kutoka Google. Kawaida mara nyingi TCL anatumia programu endeshaji yake mwenyewe ambayo haina apps nyingi, pia anatumiaga programu endeshaji inayokwenda kwa jina la Roku kwenye TV za bei ya juu (Roku imetengenezwa kwa kutumia Android pia).

Bei zake

TV hizi zinachukua sifa ya kuwa baadhi ya TV za bei nafuu zaidi kuja zikiwa na toleo la Android TV tena kutoka kwa ‘brand’ kubwa kama TCL.

INAYOHUSIANA  Bill Gates na mpango ya kujenga jiji janja kwenye jangwa

Inchi 32 inapatikana kwa dola 130 (takribani Tsh 300,000), huku ile ya inchi 40 inauzwa kwa dola 200 (takribani Tsh 465,000). Tukiamini ata zitakapopatikana hapa nchini basi bei haitakimbia sana.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Mhariri Mkuu

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. | mhariri@teknokona.com |