Kampuni kongwe katika utengenezaji wa diski uhifadhi – hard drive na usb flash drive, ya Kingston yatambulisha rasmi USB Flash Drive zenye ujazo mkubwa zaidi.

USB Flash Drive hizo zinazokuja na ujazo wa TB 1 na toleo jingine la TB 2 zitatolewa chini ya familia ya Kingston DataTraveler Ultimate GT, – GT ikimaanisha ‘Generation Terabyte’, yaani kizazi cha terabyte.
USB Flash Drive ya TB 2 itachukua rekodi ya kuwa USB Flash Drive yenye ujazo wa juu zaidi kuwahi kupatikana sokoni.
Flash Drive hizi zimetambulishwa katika maonesho ya bidhaa za elektroniki huko jijini Las Vegas, #CES2017. Zinategemewa kuingia sokoni ifikapo mwezi wa pili mwaka huu ila hadi sasa bei zake bado hazijawekwa wazi ila kwa kiasi kikubwa usitegemee ziwe bei rahisi.
Sifa zingine kwa undani;
- Ujazo: TB 1/TB 2
- Kasi: USB 3.1 Gen. 1
- Urefu na upana: 72mm x 26.94mm x 21mm
- zitaweza kufanya kazi kwenye programu endeshaji mbalimbali: Windows 10, Windows 8.1, Windows 8, Windows 7 (SP1), Mac OS 10.9.x and above, Linux v.2.6.x and above, Chrome OS