Funga na kisha tupa ufunguo kabisa. Subiri kwanza…..Lakini hakuna ufunguo!. Watengenezaji wake wanaliita kufuli janja. Makufuli ya ‘TappLock’ ambayo yapo ya aina tofauti tofauti hayahitaji ufunguo, namba za siri au hata simu ili tuu kumuwezesha mtu kuyafungua.
Mbadala wake kufuli hizi zitahitaji tuu alama ya kidole (fingerprint sensor) ambayo mtu atakuwa kahifadhi katika kufuli hilo.
Cha kufurahisha zaidi ni kwamba mtu akigusa kufuli hilo kwa lengo la kufungua, mlolongo mzima utachukua sekunde 0.8 tuu mpaka kufuli hilo kufunguka ( Achana na yale ya uswazi, likigoma mpaka uweke mafuta na uanze kutekenya tena Haha!)
Makufuli haya ya TappLock yanapatikana katika maumbo makubwa na madogo. Kufuli linakuja na sehemu ya chaji kama simu janja zilivyo, sehemu ya kuingiza chaji ni kwa chini ya kufuli hili
Akili za watu waliotengeneza makufuli haya pia waliwaza kuwa kwa upande mmoja au mwingine pia mtu anaweza akaamua kuwapa marafiki au ndugu katika familia ruhusa na kushiriki katika kulifungua kufuli hilo
Angalia Video Ukielezea Makufuli Hayo Ya Tapplock
Kwa kutumia App inayoendana na TappLock ambayo inaweza kungia katika simu janja za iOS, Windows na Android, watumiaji wanaweza kushiriki na kupeana ruhusa ya kufungua makufuli haya
Kwa mfano labda umesafiri na umeacha kitu cha rafiki yako pale nyumbani kwako. Sio tuu kwamba utaweza kumpa ruhusa ya kufungua kufuli hilo kwa kutumia App inayoendana na kufuli la TappLock bali pia unaweza hata ukaseti ni muda gani ambao unataka mtu (rafiki) huyo awe anaweza kutumia kufuli hilo (kulifungua). Kumtoa mtu katika orodha ya watumia wa kufuli hilo (TappLock) ni rahisi sana.
Kwa ujumla TappLock ina uwezo wa kuhifadhi hadi alama 200 za vidole. Kufuli hili janja la TappLock lina hadi alam ambayo imewekwa ndani yake. Mtu ambae hana mamlaka akiamua kutumia kidole chake kwa lengo la kufungua kufuli hili litapiga kelele. Bei yake ni kati ya $29-$49 kulingana na ukubwa na toleo la kufuli lenyewe.
No Comment! Be the first one.