fbpx
TeknoKona Teknolojia Tanzania

Intaneti Netflix

Tamthilia ya Squid Game ya Korea Kusini yavunja rekodi Netflix

Tamthilia ya Squid Game ya Korea Kusini yavunja rekodi Netflix

Spread the love

Tamthilia ya Squid Game iliyotengenezwa nchini Korea Kusini na kampuni ya Netflix imeendelea kupata umaarufu mkubwa mtandaoni na ata kwenye utazamaji wake kupitia huduma ya Netflix.

Mtandao huo ambao ni mara chache sana unaweka wazi data za utazamaji wa filamu na tamthilia zake, umesema tamthilia hiyo kwa sasa inashika nafasi ya kwanza kama tamthilia iliyoangaliwa zaidi katika huduma ya Netflix. Netflix wanasema hada sasa ishaangaliwa na watumiaji milioni 111, na huku ikishika nafasi ya kwanza kama tamthilia inayoangaliwa zaidi katika mataifa zaidi ya 80.

SOMA PIA  Google Waondoa Uwezo wa Watu Kufanya Mabadiliko Ktk Google Maps

Tamthilia ya Squid Game

Tamthilia ya Squid Game imeipokonya tamthilia ya nyingine ya Netflix inayokwenda kwa jina la Bridgerton iliyokuwa inashika nafasi ya kwanza.

Netflix wamesema kwa mwaka mpya wa fedha wanategemea kutumia zaidi ya dola milioni 500 katika utengenezaji wa filamu na tamthilia nchini Korea Kusini. Korea Kusini inasifika sana katika utengenezaji wa filamu na tamthilia, umaarufu wa tamthilia ya Squid Game unaweza sababisha watu wengi zaidi waanza kutazama filamu nyingi zaidi kutoka taifa hilo.

SOMA PIA  Alama 'Kidole Chini' a.k.a 'Dislike' Haitakuja Facebook ~ Zuckerberg

Tazama trailer ya Squid Game hapa,

Tamthilia hii, ambayo ni ya utunzi tuu (si ya maisha ya kweli) inaonesha jinsi baadhi ya watu wenye madeni mengi yanayoathiri maisha yao wanachukuliwa na kuwekwa kwenye kambi. Wakiwa kambini wanalazimika kushiriki michezo mbalimbali ambapo mtu akishindwa basi anauwawa. Kila mechi zinavyoendelea ndevyo pesa kwa ajili ya mshindi wa mwisho zinavyoongezeka zaidi.

SOMA PIA  EML Search: Google, Yahoo na Bing kwa Wakati Mmoja

Kuiangalia Netflix bofya hapa -> Netflix/Squid Game

Tayari wengi wanaamini kutakuwa na msimu wa pili wa tamthilia hii. Na kama ni hivyo basi tutegemee si chini ya mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu kwa msimu huo kuja.

Comrade Mokiwa

Comrade Mokiwa

Muanzilishi wa Teknokona na Teknokona Group LTD - WWW.TEKNOKONAGROUP.COM

Muda wangu umegawanyika kati ya kazi kibunifu @teknokonagroup na uandishi wa habari za Teknolojia hapa Teknokona Blog.

| mhariri(at)teknokona.co.tz |

Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

TeknoKona Teknolojia Tanzania