fbpx
Gari, Teknolojia

Sweden Imefungua Barabara Ya Umeme (eHighWay) Kwa Magari Makubwa!

sweden-imefungua-barabara-ya-umeme-ehighway-kwa-magari-makubwa
Sambaza

Pengine Sweden ndio inaweza ikawa nchi ya kwanza kuja na teknolojia hii kwa magari makubwa. Magara haya yanatembea katika barabara ambazo zimeunganishwa na nyaya za umeme

Kilichofanyika ni kwamba magari hayo kwa juu yameunganishwa na nyanya ambazo zinaelea (zilizo shikiliwa na nguzo). Jina la kitaalamu ya barabara hii ni eHighway.

Magari ambayo yanapita katika barabara hiyo ni yale makubwa kabisa na kwa sasa magari makubwa ya kampuni ya Scania ndio yanafanya majaribio katika barabara hizo

INAYOHUSIANA  Apple na Samsung Kushirikiana na Makampuni ya Simu Kukuletea E-SimCard
Magari Makubwa Mawili Moja Likiwa Linapita Katika eHighway, Lingine Katika Barabara Ya Kawaida

Inasemekana kuwa wakati yakiwa katika barabara hiyo yatakuwa hawayatumii mafuta hata kidogo, lakini yakitoka nje ya barabara hiyo ya umeme basi yatarudi katika kutumia mafuta kama kawaida

Ubunifu huu umetoka kwa kampuni ya Siemens ambayo imetoa teknolojia hii kwa magari makubwa kwa kushirikiana na kampuni ya Scania


Ripoti zilizopo ni kwamba zaidi ya theluthi ya hewa chafu (Carbon Dioxide) inatokana na vyombo vya usafiri, hivyo basi teknolojia ni njia moja wapo ya kupunguza machafuko hayo

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kuweka muonekano wa giza kwenye FB Messenger

Ukiachana na Sweden bado kampuni ya Siemens ipo katika plani za kuanzisha eHighway nyingine huko California kwa kushirikiana na kampuni ya Volvo

Majaribio ya teknolojia hii huko Sweden yatafanyika kwa kipindi cha miaka miwili na kama nchi hiyo ikiona ina manufaa kwao basi barabara nyingi za mfumo huu zitatengenezwa

ehighway
Teknolojia inazidi kukuwa kwa kiasi kikubwa sana na hivi sasa inajaribu kumeza kila kitu. Teknolojia hii ni ya aina yake na pia ni nzuri kwa nchi ambayo ina nishati kubwa ya umeme. Kwa mfano ikija kwa nchi kama Tanzania inaweza ikawa ni tatizo kwani umeme tuu ni shida

Niandikie hapo chini katika sehemu ya comment wewe jambo hili unalionaje? Na je likija katika nchi yako litafanikiwa kwa urahisi au la? Ningependa kusikia kutoka kwako.

Tembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku kwa habari na maujanja mbalimbali yanyohusu teknolojia kwa lugha ya Kiswahili. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: ,

Hashdough

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com