fbpx

Spika yenye sehemu ya kuwekea bilauri

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kutokana na ukuaji wa teknolojia katika dunia ya leo naamini kabisa umeshakutana na spika za aina mbalimbali na ili kuzifanya zivutie zaidi zinakuwa na ubunifu unaoshawishi mara moja.

Sherehe zipo za aina mbalimbali na unakuwa unaanda tafrija basi muziki una umuhimu wake ili kuwaburudisha watu na ndipo hapo unapozingatia ukubwa au udogo wa spika kulingana na shughui uliyoiandaa.

Lakini kwa teknolojia ya siku huzi spika inaweza kuwa ndogo ila muziki utakaokuwa unatoka hapo ni mkubwa kuzidi umbo la kifaa chenyewe. Mfano mzuri ni Sony GTK-PG10 ambayo kimsingi ina sifa zifuatazo:-

  • betri yake inadumu na umeme kwa saa 13 pia inaweza kuchajiwa, ina redio
  • ina sehemu ya kubadilisha ladha ya muziki/mdundo, inatumia bluetooth
  • ina sehemu ya kuwekea bilauri zisizozidi nne kwa yeyote atakayekuwa anapata kinyaji+upo uzio unaosaidia spika isidhurike iwapo mtu skikosea kuweka vizuri  bilauri yake na kumwagikia kwenye spika,
  • ina sehemu ya kuchomeka lipaza sauti, mambo ya karaoke yatawezekana.

    bilauri

    Spika kutoka Sony ya kwanza kwa mwaka 2019.

Spika hiyo ilizinduliwa kwenye onyesho la CES 2019 na bei yake ni $250|zaidi ya Tsh. 575,000. Inafaa sana kwa sherehe zinazofaniyika nje mathalani kwenye ufukwe wa bahari, viwanjani, n.k.

Vyamzo: The Verge, The Vinyl Factory

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Wanaolipia Spotify wafikia milioni 100
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.