Kampuni ya Sony imetangaza kusitisha kutoa huduma pamoja na maboresho yoyote yanayohusu Play Station 2 (PS2) maarufu kama ”Gwiji”.
Sony kwa sasa watahusika katika maboresho au kutoa huduma kwa Play Station 3 na 4 tu. PS2 ndio iliyopata umaarufu zaidi na kuuzwa kwa wingi duniani kote.
Play station 2 ilizinduliwa tarehe 4 Machi 2000 nchini Japan na baadae Oktoba Amerika ya Kaskazini na imeuzwa zaidi ya milioni 155 duniani kote. Pia ndio kifaa ambacho kina na michezo takribani 3000 ya aina mbalimbali.
Tangazo la Sony kuhusu kusitisha huduma kwa PS2 limepokelewa kwa huzuni kubwa kwa watumiaji wengi wa mchezo huo ambao walitweet katika akaunti zao kusikitishwa na hatua hiyo.
Michezo maarufu iliyokuwa ikitumika katika PS2 ni Grand Theft Auto: San Andreas, Ratchet and Clank, The Simpsons: Hit & Run, Spider-Man na bila ya kusahau mpira wa miguu.