fbpx

Sony watengeneza runinga kubwa zaidi ya upana wa basi

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Katika teknolojia ya runinga bora, kubwa na za kisasa kampuni ya Sony haiwezi kukosekana kwenye orodha na hii inatokana na utengenezaji wao ambao mara zote umekuwa ukiwafanya wapate kufahamika vyema.

Kwa mara nyingine baada ya miaka mitano Sony wametenegenza runiga kubwa zaidi ya upana wa basi na kutokea kupata mteja mara moja. Mwaka 2014, Sony walitengeneza runinga ya ubora wa 16K na kuiweka kwenye uwanja wa ndege wa Haneda, Tokyo-Japan.

Sasa hii ya mwaka huu wa 2019 ni ya 16K yenye upanda wa mita 19.2 (futi 63) na urefu wa mita 5.4/futi 17 ambapo Sony wametumia teknolojia ya Crystal LED ambapo ndani yake wakaweza kutengeneza mifumo ya LED nyingine ndogondogo inayosaidia kutengenza runingza za ukubwa/ubora wowote ule.

runinga kubwa

Runinga kubwa iliyotengenezwa na Sony yenye ubora wa 16K, inchi 783.

Kwa sasa runinga hiyo imewekwa kwenye kampuni moja ya masuala ya ubunifu wa mavazi ambapo wanatoa hamasa wau walete picha za ubora huo na kwa hakika hazitahitaji kuongezewa nakshi nakshi ili kufanya kuonekana na ung’avu wa kuvutia.

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Uvumi: Sony kuja na simu yenye display ya kukunjwa
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.