fbpx
apps, Teknolojia

Snapchat yajiandikisha katika soko la hisa! #Apps

snapchat-yajiandikisha-katika-soko-la-hisa-apps
Sambaza

Mtandao wa Snapchat siku ya Alhamisi uliingia katika vichwa vya habari vya mitandao mingi ya biashara baada ya kuanza mchakato wa kujiunga na soko la hisa, Snapchat  imejiandikisha kama SNAP katika soko la hisa la New York maarufu kama NYSE.

hisa

Snap ambayo ndiyo kampuni ya mama ya mtandao wa snapchat imeanza mchakato wa kuuza hisa zake na inategemewa kampuni hii itaweza kukusanya hadi dola za kimarekani bilioni 25, kama matarajio haya yatafikiwa basi kampuni hii itakuwa imevunja rekodi ya makampuni mengine na pengine itakuwa na thamani katika soko hatakuishinda Twitter.

INAYOHUSIANA  China wafanya majaribio ya ndege ya kwanza ya abiria kutengenezwa nchini humo

Katika taarifa yake iliyowasilishwa katika undikishaji huo Snapchat imesema kwamba hadi mwaka jana mwishoni ilikuwa na watumiaji hai milioni 158 kila siku, pia taarifa hiyo ilisema kwamba kuna takribani snap bilioni 2.5 ambazo zinatengenezwa kila siku.

Baada ya kuanzisha mchakato wa kujiandikisha katika soko la hisa kampuni hii intakiwa kuwashawishi wawekezaji ili waweze kuwekeza pesa katika hisa za kampuni hii, jambo hili sio rahisi hasa ukizingatia ukweli kwamba aina ya biashara Snapchat inafanya sio kitu watu walikizoea.

INAYOHUSIANA  Trilioni 6 imetumika kununua maongezi

Wengi walisema snapchat haitadumu, wengi walitabiri kwamba ingekufa kama ambavyo mitandao mingi inayoanzishwa hufa lakini hali haikuwa hivyo hii ni fundisho kwa wajasiriamali wadogo kutovunjika moyo pindi wachambuzi wanapo ponda mawazo yao.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus.

Habari hii imeandikwa kwa msaada wa vyanzo mbalimbali mtandaoni.

 

Facebook Comments

Sambaza
1 Comments
Share

Notice: Trying to access array offset on value of type null in /home/teknoloj/public_html/wp-content/plugins/intelly-related-posts/includes/core.php on line 163

Nickson

1 Comments

  1. Dola Bilioni 24! Snapchat yazidi kujidhatiti katika soko la hisa - TeknoKona
    March 3, 2017 at 3:52 pm

    […] Kwa zaidi ya miaka minne ya kujiendesha kama kampuni bila kutegemea pesa yoyote ile kutoka kwa watu wengi kama vile wanahisa hivi karibuni Snapchat iliamua kujiunga na soko la hisa la jijini New York. […]