fbpx
apps, Intaneti, simu, Snapchat, Teknolojia

Snapchat waonja shubiri ya kupata hasara

snapchat-waonja-shubiri-ya-kupata-hasara
Sambaza

Kampuni ya Snap Inc imekuwa haifanyi vizuri sokoni na matokeo ya taarifa ya kampuni hiyo katika kipindi cha robo ya kwanza (Q1) kwa mwaka wa fedha 2018 yalikuwa chini ya matarajio.

Matokeo ya mapato katika robo ya pili ya mwaka wa fedha yametolewa huku hali ikizidi kuwa mbaya. Katika kipindi cha kuanzia Aprili 1-Juni 30 Snap Inc iliingiza mapato ya dola za Marekani milioni 262 (Tsh. bilioni 580), hasara ikiwa ni dola za Marekani milioni 353|Tsh. bilioni 780.

INAYOHUSIANA  Simu milioni 900 za Android hatarini kudukuliwa

Kitu cha kushtusha zaidi katika ripoti hiyo ni anguko kubwa la akaunti za Snapchat kuhusu watumiaji wa kila siku, ambapo idadi hiyo imeporomoka kutoka milioni 191 katika robo ya kwanza (Q1) hadi milioni 188 katika robo ya pili (Q2).

Sababu kubwa ya anguko hilo imetajwa kuwa ni mkanganyiko wa mabadiliko na muundo mpya wa programu tumishi (Snapchat) ya kampuni hiyo huku ikiwa mara ya kwanza kwa idadi ya akaunti za Snapchat kushuka tangu Snap Inc ijitambulishe kwa umma.

Licha ya kuporomoka vibaya kwa idadi ya watumiaji, Snap Inc imeripoti kuwapo kwa hasara kidogo tu katika thamani ya hisa zake tofauti na vile ilivyotarajiwa na wawekezaji na mpaka  Agosti, 10 2018 mauzo ya hisa zake yaliogezeka kwa asilimia 11. Bei ya kila hisa moja kwa Snap Inc kwa sasa ni $13.12|Tsh. 29,000.

kupata hasara
Wastani kila siku wa Snapchat duniani imeongezeka kwa 8% pekee.

Imepita takribani miezi sita sasa tangu kubadilishwa kwa muundo wa Snapchat huku wahusika wakisema wataifanyia maboresho programu hiyo kulingana na maoni ya watumiaji.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share
Tags: , ,

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.