fbpx

Snapchat waanza kuuza Miwani za kurekodia video huko Marekani

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Snapchat imeanza kuziuza miwani zake maalumu za kurekodia video kupitia mtandao, awali miwani hizi zilikuwa zinauzwa kupitia maduka maalumu ambayo yaliwekwa katika miji tofauti tofauti.

Marekani.

Miwani hizo ambazo zinaanza kuuzwa.

Snapchat wanauza miwani hizi katika mtandao kwa watumiaji walio Marekani kwa dola za Marekani 129.99 kila moja, hii inaweza kuwa nimoja kati ya mbinu za kampuni hii kuwathibitishia wawekezaji kwamba kuna njia nyingine ya mapato na sio tu kupitia matangazo.

INAYOHUSIANA  Ndege ya kwanza inayotumia umeme yarushwa China

Mtandao huu umekuwa katika harakati za kuwavutia wawekezaji tangu ulipotangaza kuuza hisa zake, hivyo inajaribu kuwavutia wawekezaji kwa kuonesha fursa zilizopo.

marekani

Mashine za kuuzia miwani hizo ambazo zilikuwa zinatumika kabla ya bidhaa hiyo kuanza kuuzwa mtandaoni.

Kabla ya kuanza uuzwaji wa miwani hizi katika mtandao Snapchat walikuwa wanatumia vibanda maalumu ambavyo vilikuwa vinachomoza katika miji mbalimbali. Hatua hii inaifanya Snapchat kuzidi kujidhatiti kimapato kwa kuongeza njia ya ukusanyaji wa mapato, tofauti na mitandao kama Instagram ambayo kwa kiasi kikubwa inategemea matangazo.

INAYOHUSIANA  WhatsApp: Tumia 'Vikatuni' vya Rangi ya Ngozi Utakayo

Kwa sasa wanaoweza kuagiza miwani hizo ni watumiaji walio nchini Marekani, kwa watumiaji walio katika nchi nyingine watahitaji kuendelea kusubiri huenda siku za usoni Snapchat wataongeza nchi ambazo watumiaji wanaweza kuagiza miwani hizo. Miwani hizi zinatumiwa kwaajiri ya kurekodia video kisha kusambaza katika mtandao huo wa Snapchat.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.