fbpx
apps, Mtandao wa Kijamii

Utafiti: Snapchat ndio mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana Marekani

snapchat-ndio-mtandao-unaoongoza-kutumiwa-na-vijana-marekani
Sambaza

Mtandao wa kijamii Snapchat ndio maarufu na unaopendwa zaidi kwa vijana wa Marekani kuliko zamani, kulingana na utafiti mpya kutoka kampuni ya uwekezaji ya kimarekani ya investment firm Piper Jaffray na pia data za kampuni nyingine eMarketer zinaonesha hivyo hivyo.

app ya snapchat

Tafiti ya Piper Jaffray inaonesha vifuatavyo;

  • Asilimia 82% ya vijana waliofanyiwa utafiti wameonesha kupendelea kuwa na simu ya iPhone. Aidha katika utafiti huo ulihusisha pia mitandao ya kijamii ya Facebook, Snapchat na Twitter.
  • Mtandao wa snapchat umeonesha kupendwa zaidi ya mingine. Matokeo hayo ya kuvutia yanaonesha asilimia 47 ya vijana wanatumia Snapchat.
  • Katika utafiti huo mtandao wa Instagram unafatia kwa kupendwa na vijana wa Marekani kwa asilimia 27, huku mtandao wa Facebook ukishika nafasi ya tatu kwa kutumiwa na vijana kwa asilimia 9.
  • Mtandao makini wa watu makini wa Twitter umeshika nafasi ya mwisho kwa kutumiwa na vijana kwa asilimia 7 tu.
INAYOHUSIANA  Instagram Wapo njiani kubadilisha namna Tunaona Posts
Snapchat ndio mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana wa Marekani
Snapchat ndio mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana wa Marekani: Utumiaji wa SnapChat (idadi ni katika mamilioni), kutoka chanzo kingine *eMarket
Snapchat ndio mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana wa Marekani
Snapchat ndio mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana wa Marekani: Utumiaji wa SnapChat ndio unazidi kukua zaidi ukilinganisha na huduma zingine.

Utafiti huo umewahusu vijana wa kuanzia umri wa miaka 16 na kaya zenye kipato cha kawaida katika majimbo ya marekani. Utafiti huo umefanywa na kampuni ya kimarekani ya investment firm Piper Jaffray.

Pia data za eMarket zinaonesha ya kwamba wakati mtangazaji anaweza kufikia vijana wa kundi la umri wa miaka 13-24 milioni 25 hadi 26 kwa siku akitangaza katika mtandao wa Facebook namba hiyo inakuwa kubwa zaidi kama akitangaza kwenye app ya SnapChat ambapo atafikia zaidi ya vijana milioni 26 wa kundi hilo hilo la umri. Hii inamaanisha ingawa Facebook inawatumiaji wengi zaidi bado SnapChat ndio watumiaji wake wanaingia mara kwa mara kwa siku. – FT.com

INAYOHUSIANA  Baada ya siku na miezi kadhaa Apps za HTC zarudi Google PlayStore

Kwa Tanzania katika utafiti usio rasmi mtandao unaoongoza kutumiwa na vijana wengi ni Facebook na Instagram ukifuatiwa na Twitter na SnapChat.

Facebook Comments

Sambaza
0 Comments
Share

Siyan

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.