fbpx

Snapchat Kuleta ‘Link’ Na ‘Background’ Katika Stories!

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +
Sambaza

Kama wewe ni mtumiaji mzuri wa Snapchat basi kaa mkao wa kula kwani mtandao huo nguli wa picha na video zinazopotea baada ya muda umekuja na vipengele vipya viwili.

Snapchat ndio mtandao ulioleta mapinduzi makubwa katika mitandao mingine katika swala zima la Stories. Mitandao mingi kwa kipindi cha nyuma ilikua haina kipengele hicho lakini Snapchat walipoanza kukitumia ndipo makampuni mengi yakaanza kukiiga,

Vipengele Vipya Katika SnapChat

Licha ya kuwa vipengele vingi vya Snapchat huwa vinanakiliwa na kutumika katika mitandao mingine hilo haliwarudishi nyuma kabisa

INAYOHUSIANA  Simu rununu Nokia 7.1 imezinduliwa

Sasa wanatoka na kipengele cha ‘Link‘ ambapo mtu unaweza ukaweka link ya mtandao wowote ndani ya post (story) zako. Mwanzoni ulikua unaweza kuweka link pale tuu unapomtumia mtu Snap (Meseji).

Kipengele Cha Link

Kingine ni kipengele cha ‘Background‘ yaani hapa utaweza kuwezesha hili kwa kutoa eneo la mbele ya Snap yako ili background ionekane.  Filter hii ya background itakuwa inabadilika kila siku kama vile zilivyo zile ‘Lense’ za kuvaa kwa mfano ile ya mbwa.

Kipengele Cha BackGround

Ukiachana na hivi vipengele vikubwa viwili, kuna taarifa zingine za kwamba kwa mara ya kwanza unaweza ukatumia ‘Voice Filters’ (Kubadili sauti) bila ya kuwa umevaa ‘lense’

Kipengele Cha Voice

Vipengele hivi bado havijatoka kila kona ya dunia ila kaa tayari kuvipata kwa siku chache zijazo.

INAYOHUSIANA  Ndege Ndogo Yakamatwa Ikiwa Inasafirisha Bangi Gerezani

Ningependa kusikia kutoka kwako, kama wewe ni mpenzi wa Snapchat niambie hii unaipokeaje? niandikie hapo chini sehemu ya comment,

Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!,

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa TeknoKona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Naomba Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.