fbpx

Skype yazindua mfumo wa usiri

Google+ Pinterest LinkedIn Tumblr +

ICT CONFERENCE 2019

Sambaza

Baada ya miezi kadhaa ya kazi, hatimae waendeshaji wa programu ya Skype wamefanikisha mawasiliano yote ya watumiaji wake kuwa ni siri.

Skype kama programu zingine kadhaa nao wameanza rasmi kutumia mfumo wa end-to-end encryption ambapo maana yake ni kwamba mawasiliano baina ya watu wawili au zaidi yanabaki kuwa salama na kuonekana kati yao tuu na si kwa wahusika wa programu au mtu mwingine wa ziada.

INAYOHUSIANA  Jinsi ya Kudhibiti Simu Yako

Pia watumiaji wa Skype wataweza kuficha mawasiliano yao yote kwa mtu mwingine kuyaona hata pale watakapoacha kufuta ujumbe au mazungumzo kwa njia ya sauti katika vifaa vyao.

Hatua hii ya kutumia mfumo wa usiri itawafurahisha watumiaji wengi ambao kwa muda mrefu walikuwa na wasiwasi wa usalama wa mawasiliano yao wanayoyafanya kupitia programu hiyo ya Skype.

mfumo

Uzuri wa Skype ni kwamba mtumiaji hata akibadilisha kifaa kimoja kwenda kingine bado mawasiliano yake yote ataweza kuyakuta kama kawaida bila ya usumbufu wowote.

Skype imekuwa programu inayopatikana katika mifumo endeshi takribani yote muhimu kuanzia kwenye simu za Android, iOS pamoja na kompyuta kwa mfumo wa Windows.

Skype ndio programu maarufu zaidi duniani kwa kupiga simu za intaneti kwa njia ya picha mnato na sauti. Hata vyombo vingi vya habari duniani huitumia kufanya mazungumzo na waandishi/watu wengine wao walio mbali na kituo cha televisheni husika.

Facebook Comments

Sambaza

ICT CONFERENCE 2019

Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.