fbpx

Simu za Samsung zinazouza kwa sana India

0

Sambaza

Samsung nchini India imetangaza kwa vyombo vya habari kuwa imeuza simu milioni 2 za Galaxy J6 na Galaxy J8 ambazo zimezinduliwa karibuni.

Kupitia Makamu Rais Asim Warsi wa Samsung India, kampuni hiyo ilidai kuwa aina za simu hizo zilivutiwa wateja wengi hivyo kufikia mauzo ya simu 50,000 kwa siku tangu uzinduzi wa J6 mwezi Mei 22 na J8 mwanzoni mwa mwezi Julai.

Mafanikio hayo yametokana na falsafa yao ni kuweka masikio yao kwa wateja na kutekeleza kile wanachotaka na kupendekeza kukiona kwenye simu zao za Samsung.

Simu za Samsung

Simu za Samsung ambazo zinafanya vyema kimauzo nchini India

Samsung Galaxy J6 ilikuwa simu yenye bei nafuu yenye kioo cha AMOLED, prosesa ya Exynos 7870, ukubwa wa uhifadhi wa 32GB na ikiwa na kamera ya 13MP.

INAYOHUSIANA  Unajua undani wa Honor V20?

Kwa upande wa Galaxy J8 inakuja na kamera mbili za nyuma 16MP+5MP, betri lenye 3,500mAh, RAM 4GB, uhifadhi wa ukubwa wa 64GB na prosesa ya Snapdragon 450.

Simu za Samsung (Galaxy J6 na J6) zimetengenezwa kwenye kiwanda cha Samsung-Noida kilichopo nchini India kilichofunguliwa mapema mwezi Julai na kuwa moja ya kiwanda kikubwa zaidi duniani cha uzalishaji wa simu.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.