Karibu miongo miwili iliyopita simu za mezani zilikuwa zikitumika sana sehemu nyingi duniani na Tanzania ikiwemo kwani simu za mkononi zilikuwa hazina umaarufu sana na utandawazi uliwa haujatanuka kabisa lakini hivi leo mambo ni tofauti kabisa.
Tukiongelea kuhusu simu za mezani unaweza ukaamini kuwa zimepitwa na wakati au hazihitajiki tena katika ulimwengu wa sasa lakini kwa maoni yangu naweza kusema bado zina nafasi nzuri tu ya kuendelea kutoa huduma zaidi ya kupiga/kupokea simu.
TTCL ambayo ndio kampuni ya simu mama na nguli nchini Tanzania inataka kuuaminisha umma kuwa simu za mezani bado zina kazi yake na kutokana na utandawazi matumizi ya intaneti yanaongezeka kila siku.
Kampuni kubwa au ndogo zinaweza kuwa moja ya wateja wa kubwa wa simu hizi hasa kwenye matumizi ya intaneti kutokana na gharama za kupata huduma hiyo zinahimilika kabisa kwa asilimia kubwa tu.
Kwa uchache tu kuhusu mchanganua wa kasi ya intaneti
Kama wewe kampuni yako ina simu/kompyuta au kifaa chochote kinachotumia intaneti (kwa idadi kuanzia 1-5) kwenye ofisi yako basi itanteti yenye kasi ya 2MBps itakufaa sana na utafurahia ineti yenye kasi kweli ya 4G.
Kumbuka wingi/uchache wa vifaa unaathiri kasi ya intaneti hivyo kama wewe ofisi mna vifaa vya kidijiti vingi na vyote vinatumia intaneti ya ofisini (kuanzia 5 na kuendelea) ni vyema mkanunua kifurushi cha juu kidogo.
Chanzo: TTCL
One Comment
Comments are closed.