Google wanajivunia sana kutokana na simu za Google Pixel ambazo zilipata mapokezi mazuri na kuifanya Google kujipatia kipato kizuri lakini pia kuiweka kwenye ramani ya ushindani kuhusu simu janja.
Kwa mwaka na zaidi sasa habari za makampuni kuweka kipengele cha “Muonekano wa giza” kwenye programu tumishi, tovuti n.k sio jambo geni sana kwa wengi, Google ambao ndio wenye simu zinazoitwa Google Pixel (Pixel 2, 2XL, 3, 3XL) wameamua kuleta masasisho ya ulinzi kwa mwezi Machi ambayo yanajumuisha muonekano wa uso mbele kwenye simu kuwa giza pamoja na kuweza kuona ni asilimia ngapi ambazo zimeshashushwa.
Kwanini muonekano wa giza?
Hilo ni swali ambalo naamini kwa yeyote ambae anapenda kujua vitu vya kidijiti atakuwa ameshajiuliza mara kadhaa na pengine akakosa jibu lakini fahamu kuwa utakapokuwa umeamua kutumia muonekano wa giza basi unaifanya simu husika kutunza chaji kwa muda mrefu zaidi kutokana na kwamba mwanga utakaokuwa ukitumika ni mdogo sana/usitumike kabisa.

Unaweza ukawa unapenda kuweka simu yako kwenye muonekano wa giza lakini ikawa changamoto kutumia prgramu tumishi fulani fulani ambazo nazo zina mbwembwe kama hizo. Sasa maamuzi ni yako lakini kiujumla kwenye Android 9 kipengele hicho kipo.
Chanzo: Android Police